Habari za Punde

Wizara ya Elimu Zanzibar Imeunda Kikosi Kazi kwa Tafiti Mbalimbali.

Wiziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Lela Muhammed Mussa akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali Zanzibar kuhusiana na Ujenzi wa Skuli na Maabara, mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Wizara mazizini Unguja.   

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imeunda kikosi kazi cha mageuzi ambacho kitaweza kusaidia kuleta mabadiliko katika sekta ya elimu nchini.

Akizungumzana waandishi wa habari juu ya mpango kazi wa wizara hiyo waziri wa elimu na mafunzo ya amali Mhe.Lela Muhammed Mussa amesema Kikosi hicho chenye wajumbe 10 kitaweza kufanya kazi kwa kutumia Tafiti mbalimbali juu ya mfumo wa elimu nchini na kuondosha kasoro Zilizopo katika  sekta hiyo.

Amesema kuwa kikosi hicho kitafanya uchambuzi wa kina kwa kuwasilisha ripoti ya matatizo yaliyopo pamoja na kuweka mikakati ya kukabiliana nayo. 

Akizungumzia kuhusu ujenzi wa skuli na maabara amesema katika mwaka fedha 2021/2022 wizara ina mpango kujenga skuli kumi na mbili pamojq maabara za kisasa kwa unguja na pemba

Hivyo ameziagiza skuli zote  za zanzibar kuhakikisha Wanawaelimisha wanafunzi juu ya umuhimu sensa ya watu na makaazi ilikushiriki katika zoezi hilo.
Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari Zanzibar wakimsikiliza Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Lela Muhammed Mussa.(hayupo pichani) wakati wa mkutano wake na waandishi uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Elimu Mazizini Unguja Jijini Zanzibar.
Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari Zanzibar wakimsikiliza Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Lela Muhammed Mussa.(hayupo pichani) wakati wa mkutano wake na waandishi uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Elimu Mazizini Unguja Jijini Zanzibar.
Mwandishi wa habari wa Gazeti la Habari leo Ndg.Khatib Suleiman (Gurecha) akizungumza na kuuliza swali wakati wa mkutano wao na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Muhammed Mussa.(hayupo pichani) uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Elimu Mazizini Unguja Jijini Zanzibar. 
Mwandishi wa habari wa Kituo cha ITV /Redio One Ndg. Farouk Karim akizungumza na kuuliza swali wakati wa mkutano wao na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Muhammed Mussa.(hayupo pichani) uliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Elimu Mazizini Unguja Jijini Zanzibar. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.