Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Awasili Nchini Burundi Kuhudhuria Sherehe za Miaka 60 ya Jamhuri ya Burundi.

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amewasili Burundi na kupokelewa na Waziri anayeshughulikia masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Vijana, Michezo na Utamaduni wa Burundi Balozi Ezéchiel Nibigira katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Melchoir Ndadaye Bujumbura. 

Rais Mwinyi anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru wa Jamhuri ya Burundi zitakazofanyika kesho tarehe: 01 Julai, 2022.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amewasili Nchini Burundi kwa ajili ya kushiriki Sherehe za miaka 60 ya Jamhuri ya Burundi zitakazofanyika kesho 01 Julai nchini humo.

 Rais Dk. Mwinyi akiwa ameambatana na Mkewe Mama Mariam Mwinyi,Mawaziri wa SMT na SMZ na Viongozi wa Taasisi mbalimbali,katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Melchior Ndadaye jijini Bujumbura wamepokelewa na Viongozi mbalimbali wa ngazi za juu wa Burundi wakiongozwa na Waziri anaeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki ,Vijana,Michezo na Utamaduni Balozi Ezechiel Nibigira pamoja na Balozi wa Tanzania nchini humo Dkt.Jilly E.Maleko

Rais Dk.Mwinyi alipita katika ya Gwaride maalumu la Heshima lililoandaliwa kwa ajili yake kiwanjani hapo.

Katika sherehe hizo za miaka 60 ya Uhuru wa Jamhuri ya Burundi,Rais Dk.Hussein Ali Mwinyi anamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.

Rais Dk.Hussein Ali Mwinyi pia anatarajiwa kukutana na kufanya Mazungumzo na Mwenyeji wake Rais wa Burundi Evariste Ndayeshimiye katika ikulu ya Burundi iliyopo jijini Bujumbura 

Taifa la  Burundi linaadhimisha kumbukumbu ya miaka 60 tokea taifa hilo lilipojipatia Uhuru wake kutoka kwa wakoloni wa Ubelgiji Julai 1, 1962.

Imetayarishwa na Idara ya Mawasiliano,

 Ikulu Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.