Habari za Punde

Wizara ya Afya Zanzibar Yakabidhiwa Vifaa Kwa Ajili Kufuatilia Maradhi ya Malaria.

Naibu Waziri wa Afya Hassan Khamis Khalfan akipokea kifaa cha kupimia malaria kwa Mkurugenzi   wa Afya  kutoka shirika la msaada Marekani (USAID) Ananthy Thambinayagam katika Ofisi ya Malaria Mwanakwerekwe Mjini Zanzibar
Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Hassan Khamis Khalfan (Kulia)akipokea Msaada wa Laptop kutoka kwa Mkurugenzi  Afya  wa shirika la msaada wa  Marekani (USAID) Ananthy Thambinayagam  hafla iliofanyika katika ukumbi wa Malariya Mwanakwerekwe Mjini Zanzibar.
Naibu Waziri wa Afya Hassan Khamis Khalfan (mwenye tai nyekundu)akikata utepe kuashiria mapokezi ya Pikipiki zilizotolewa Msaada na Shirika la Msaada la Marekani (USAID) kwa ajili ya kufatilia Maradhi ya Malaria katika Vijiji ,hafla iliofanyika katika Ofisi ya Malaria Mwanakwerekwe.wakwanza kushoto(mwenye koti jeupe)Mkurugenzi Afya wa Shirika la Msaada Marekani Ananthy Thambinayagam na (katikati) Mwakilishi wa Shirika la Msaada wa Malaria Dk.Chonge Kitojo.
Naibu Waziri wa Afya Hassan Khamis Khalfan akipatiwa maelezo na Mkuu wa Huduma za Uchunguzi wa Vimalea vya Malaria Zanzibar Safia Mohammed Ali wakati alipotembelea katika Ofisi ya Malaria Mwanakwerekwe Zanzibar.
Naibu Waziri wa Afya Hassan Khamis Khalfan akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kukabidhiwa Vifaa mbalimbali kwa ajili ya maswala ya Afya hafla iliofanyika katika Ofisi ya Malaria Mwanakwerekwe Zanzibar.
PICHA NA Miza Othman -Maelezo Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.