Habari za Punde

MAJALIWA AFUNGUA KONGAMANO LA NNE LA KIMATAIFA LA NISHATI TANZANIA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Nishati, January Makamba katika Kongamano la Nne la Kimataifa la Nishati Tanzania  alilolifungua kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere mkoani Dar es salaam, Agost 3, 2022.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Kongamano la Nne la Kimataifa la Nishati Tanzania  kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere mkoani  Dar es salaam
Baadhi ya washiriki wa Kongamano la Nne la Kimataifa la Nishati Tanzania wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipofungua kongamano hilo  kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere mkoani Dar es salaam.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akitazama chombo kinachoonyesha ramani ya kiwanda cha kuchakata gesi asilia kinachotarajiwa kujengwa mkoani Lindi wakati alipotembelea banda la makampuni ya Shell na Equinor  baada ya kufungua Kongamano la Nne la Kimataifa la Nishati Tanzania  kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere mkoani  Dar es salaam, Agost 3, 2022.  Kulia ni Makamu wa Rais na Meneja wa Kampuni ya Uquinor nchini, Unni Merethe Fjaer na katikati ni Makamu wa Rais na Mwenyekiti wa Kampuni ya Shell nchini,  Jared Kuehi.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.