Habari za Punde

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akutana na Kuzungumza na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo, Kinshasa nchini humo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mhe. Jean-Michel Sama Lukonde Kyenge mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa N’Dijili Kinshasa nchini DRC kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 42 wa Wakuu wa nchi na Serikali wa SADC utakaofanyika tarehe 17 Agosti, 2022 nchini humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo mara baada ya kuwasili katika Jiji la Kinshasa tarehe 16 Agosti, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mhe. Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo mara baada ya kuwasili Kinshasa nchini DRC tarehe 16 Agosti, 2022.
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.