RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Wananchi na Ndugu katika
kisomo cha hitma na dua kumuombea Kaka yake Marehemu Hassan Ali Hassan Mwinyi iliyofanyika
kijijini kwao Mangapwani Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja na (kushoto kwa Rais) Mtoto wa Marehemu
Ibrahim Hassan Ali Hassan, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Alhaj Othman
Masoud Othman na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhaj Hemed Suleiman
Abdulla, wakijumuika katika kisomo hicho leo 31-8-2022.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Wananchi na Viongozi
mbalimbali wa Serikali na Vyama vya Siasa katika Sala ya Jeneza ya Marehemu
Hassan Ali Hassan Mwinyi Kaka yake iliyofanyika Kijijini kwao Mangapwani Wilaya
ya Kaskazini “B” Unguja leo 31-8-2022, na (kulia kwa Rais) Rais Mstaafu wa
Tanzania Alhaj Ali Hassan Mwinyi,Mbunge wa Jimbo la Mahonda Mhe. Abdalla Hassan
Mwinyi na Spika wa Baraza la Wawakilishi
Alhaj Zuberi Ali Maulid
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na kupewa mkono wa pole na
Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Mhe. Zito Zuberi Kabwe, wakati wa maziko ya
Kaka yake Marehemu Hassan Ali Hassan Mwinyi yaliyofanyika Kijiji kwao Mangapwani
Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja leo 31-8-2022
RAIS Mstafu wa Tanzania Alhaj Ali Hassan Mwinyi
akiweka mchanga katika kaburi la Mtoto
wake Marehemu Hassan Ali Hassan Mwinyi maziko yaliofanyika leo 31-8-2022 Mangapwani
Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja leo 31-8-2022
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akiweka mchanga katika kaburi la Marehemu
Kaka yake Hassan Ali Hassan Mwinyi, wakati wa maziko hayo yaliyofanyika leo 31-8-2022
katika Kijiji cha Mangapwani Wilaya ya Kaskazini “B”Unguja
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akishiriki katika kuitikia dua ya kumuombea Marehemu Hassan Ali Hassan
Mwinyi ikisomwa na Sheikh Shariff (hayupo pichani) baada ya kumalizika kwa
maziko hayo yaliyofanyika katika Kijiji cha Mangapwani Wilaya ya Kaskazini “B”
Unguja leo 31-8-2022 na (kushoto kwa Rais) Rais Mstaafu wa Tanzania Alhaj Ali
Hassan Mwinyi, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Alhaj Hemed Abdulla Suleiman na Rais Mstaafu wa Zanzibar Alhaj
Dkt.Amani Karume
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na kuagana na Rais Mstaaf wa
Zanzibar Alhaj Dkt.Amani Karume, baada ya kumalizika kwa maziko ya Kaka yake
Marehemu Hassan Ali Hassan Mwinyi yaliyofanyika katika Kijiji cha Mangapwani
Wilaya ya Kaskazini “B” Unguja leo 31-8-2022, na (kushoto kwa Rais) Mufti Mkuu
wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhaj
Hemed Abdulla Suleiman
No comments:
Post a Comment