Habari za Punde

Serikali imeweza kutekeleza programu za kustawisha wananchi - Soraga

  

NA ALI ISSA NA PILI ALI -MAELEZO 22/08/2022


WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Mudrik Ramadhan Soraga, amesema wizara imetekeleza programu mbali mbali katika kuhakikisha serikali inastawisha utendaji mzuri kwa wananchi wake.


Waziri Soraga aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.


Alisema utekelezaji huo uliofuata sheria ya kazi na sera zilizopo ili kuona inatimiza malengo iliyojiwekea .


Alisema suala la ajira limepitiwa na sera ili  kuwajengea uwezo vijana wao na kuweza kuajirika katika sekta mbali mbali ikiwemo ajira za ndani na za nje ambapo hadi sasa wameweza kuratibu vijana 98 katika kupata ajira katika nchi za kiarabu ikiwemo Kuwait, Oman Saudi Arabia, Dubai na nchi zengine.


Aidha alisema wameweza kutoa ajira za ndani zipatazo 2008 ikiwemo ualimu, ulinzi, afya na mahoteli katika mashirika binafsi hapa nchini.


Alisema pia katika programu hiyo wameweza kutoa mafunzo kwa vijana 90 katika mafunzo ya useremala, masuala ya utalii ambapo vijana 39 wamenufaika na mafunzo hayo.


Alisema amekagua sehemu za kazi mbali mbali kutizama usalama na afya kazini katika sekta 28 ambazo zilizosajiliwa sambamba na  ukagua wa taasisi binafsi 28 za kazi na kubainika kwamba taasisi  8 hazizingatii ulipaji wa mishahara ya kima cha chini kwa wafanyakazi wao..


Alisema kwa wale waajiri ambao bado hawajalipa kima cha chini cha mshahara, hivyo serikali imeweka jopo maalumu la ufatiliaji akiwemo shirikisho la wafanyakazi, shirikisho la waajiri kwa lengo la kupatikana ufumbuzi.

.

“Serikali inatambua kuwa kuna baadhi ya Taasisi haziwezi kulipa kima cha chini cha mshahara kwa shilingi laki tatu kama lilivyotolewa agizo na Serikali,  kwa mfano mpika chipsi wa forodhani si rahisi kumlipa laki tatu mfanyakazi wake,  hivyo wamewataka kwenda Taasisi husika kupeleka malalamiko yao ili kuliangalia suala hilo”alisema.


Soraga, akizungumzia suala la Mikopo Wizara ya Uwezeshaji wananchi kiuchumi amesema serikali imetenga zaidi ya shilingi Bilioni 31 ili kuwawezesha wananchi kiuchumi.,


Alisema kwa upande wa Wizara imetoa mikopo Milioni 55 kwa Unguja na Pemba ili kuwawezesha wananchi wao na kuona wanapiga hatua kimaisha.


Alisema mpaka sasa wameweza kutoa mikopo katika vikundi 640 ambapo yenye kiasi cha shilingi Bilioni 6.6 Unguja na Pemba ikiwemo vikundi vya wajasiriamali , mboga mboga boda boda na wakulima wa mwani.


Alisema changamoto kubwa hapo mwanzo katika upatikanaji mikopo ni usimamizi mdogo katika sehemu za wilaya jambo ambalo limezorotesha upatikanaji wa mikopo hiyo.


Alisema kutokana na changamoto hiyo serikali imeweka kituo cha One Stop Centre kwa kila wilaya ili kuendelea kuwatambua wananchi wao na kuwapatia mikopo bila usumbufu vile vile wanawashirikisha watu wa CRDB na Wakuu wa Wilaya.


Akizungumzia suala la vyama vya ushirika alisema jumla ya vyama vya ushirika 1316 vimeweza kusajiliwa kwa Unguja na Pemba ambapo Unguja 976 wamesajili na kwa Pemba 140 .


Alisema kupitia vyama hiyo Wizra imeweka mikakati yake kuhakikisha watawapatia mafunzo wajasiriamali wote ili waweze kuendesha biashra zao na kuweza kurejesha mikopo kwa wakati


Alisema kumekuwa na mwamko mkubwa  baada ya kusikia  kuwepo fedha za Covid 19 wananchi wengi wameweza kuhamasika kujitokeza kuunda vyama vyao ambapo zoezi hilo limeongeza vyama vilivyosajiliwa na kufikia 89600.


Alisema akizungumza kwa upande wa program katika wizara yake wanajumla ya program mbili ambapo zipo chini ya wizara ambapo moja inaitwa Beer foot Collage iliyopo Kinyasini hii ni program inayowasaidia wajasiriamali kinamama ambao hawajui kusoma wala kuandika kwa kuwajengea uwezo wa kutengeneza taa za jua, solar .


Alisema program hii imeweza kutanua wigo ikiwemo shughuli za uzalishaji  nyuki , sabuni , utengenezaji fanicha program ambayo inafanya kazi vizuri hasa kuendelea kusadia wizara na kutilia mkazo ufugaji wa nyuki.


Alisema katika kipindi hiki wameweza kuwasaidia utaalamu wafugaji nyuki 100 wamepewa mafunzo kwa mkoa mjini Magharibi,  Kaskazini na Program nyengine kutoka Karume cha kuwalea wajasiriamali huko Mbweni  kwa lengo la uchakataji wa bidhaa kwa wajasiriamali  wanaofanya shughuli zao.


Alisema kituo hicho kimeweza kutoa mafunzo kwa wajasiriamali 500 wanaume na wanawake Unguja na Pemba.


Akizungumza suala la uwekezaji Waziri huyo alisema hadi sasa tayari wameshajitokeza wawekezaji sita ambao wameshaelekeza kutaka kuekeza katika masuala mbali mbali na hivi sasa wako katika mchakato wa mazungumzo..


Alisema hali ya uwekezaji hivi sasa inaendelea  vizuri kwa kuwajengea uwezo watendaji wake ili kufanyakazi kwa ufanisi .

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.