Habari za Punde

Matumizi mazuri ya Vibanda vya Simu vyageuzwa sehemu za dharura

Hiki zamani kilikuwa kibanda cha simu lakini sasa imekuwa ni kituo cha kuhifadhia mashine ya Defibrillator katika miji ya Uingereza
Defibrillator ni mashine maalum ambayo hutumika wakati wa dharura hutoa mionzi mikali ya umeme ( high energy electrical shocks) ili kumsaidia kwa haraka aliepata mshtuko wa moyo na kupelekea moyo wake kusimama
Zimewekwa kwenye vibanda vya simu ili viwe karibu na watu hasa ikitokea mtu amepatwa ghafla na mshtuko wa moyo. Ni mbadala wa CPR yaani pale tunapojaribu kumbinya kifua mgonjwa ili tuurudishe moyo wake kwenye kusukuma damu.

Hii ni kama huduma ya kwanza huku ukitakiwa kupiga simu 999 kwa ajili ya kuita Ambulance
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.