Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Amewaaga Madaktari Bingwa Kutoka Jamhuri ya Watu wa China Wanaomaliza Muda wao wa Kazi Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Timu ya Madaktari Bingwa kutoka Jamhuri ya Watu wa China, walipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wao wa kazi Zanzibar katika Hospitali za Unguja na Pemba, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu leo 10-9-2022
MADAKTARI Bingwa kutoka Jamhuri ya Watu wa China  wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) akizungumza wakati wa hafla ya kumuaga baada ya kumaliza muda wao wa kazi Zanzibar katika Hospitali za Unguja na Pemba, mazungumzo  yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 10-9-2022
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa Tuzo Maalum na Kiongozi wa Madaktari Bingwa kutoka Jamhuri ya Watu wa China Dr. Qu, iliyotolewa na Timu ya Madaktabi Bingwa wa China, walipofia Ikulu Jijini Zanzibar leo 10-9-2022, kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza muda wao wa Kazi Zanzibar katika hospitali za Unguja na Pemba 

WAZIRI wa Afya Zanzibar Mhe.Nassor Ahmed Mazrui akizungumza katika hafla ya kuwaaga Madaktari Bingwa kutoka Jamhuri ya Watu wa China  baada ya kumaliza muda wao wa Kazi Zanzibar, kutowa huduma za Afya kwa Wananchi katika Hospitali za Unguja na Pemba, mazungumzo hayo yaliyoyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 10-9-2022

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimvisha nishani  mmoja wa Madaktari Bingwa kutoka Jamhuri ya Watu wa China, wanaomaliza muda wao wa Kazi Zanzibar wa kutowa huduma za  matibabu katika Hospitali za Unguja na Pemba, walipofika Ikulu Jijini Zanzibar leo 10-9-2022, kwa ajili ya kumuaga


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.