Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk Hussein Mwinyi amewataka Watanzania na Waafrika kwa
ujumla kuunga mkono jitihada za Serikali zao za kuhamasisha kununua huduma na
bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya ndani ya Afrika.
Mhe. Rais
Mwinyi ameyasema hayo jijini Dar es Salaam katika Hotuba iliyosomwa kwa Niaba
yake na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, alipofunga
Mkutano wa kimataifa wa Wanawake na Vijana katika Bishara chini ya Mkataba wa Eneo Huru la Biashara Afrika.
Mhe. Mwinyi amesema kwamba hatua hiyo ya kupenda
bidhaa za ndani itasaidia kutimiza malengo ya Biashara chini ya Mkataba wa Eneo
huru la Biashara Afrika ya kukuza bishara na Viwanda Barani Afrika katika
jitihadaza kukuza na kuenua uchumi na maendeleo kwa jumla.
Amesema kewamba Kaulimbiu ya
mkutano huo ya "Wanawake na Vijana ni Injini ya Biashara chini ya Mkataba wa Eneo
Huru la Biashara la Afrika, iwapo itatekelezwa kwa vitendo itachangia sana wanawake
wengi zaidi kushiriki katika shughuli za biashara na kupelekea uchumi kuimarika na kukua zaidi.
Amefahamisha kwamba kuwepo ushiriki
mkubwa wa wanawake kwenye mkutano huo ambao umafanyika sambamba na maonesho ya
kibiashara ni unaonesha umuhimu kwa nchi
za afrika katika kuona ushiriki bora wa wanawake kwenye harakati za biashara
kwa lengo la kukuza uchumi na maendeleo yao.
Amesema kwamba mkutano huo
umeonesha kuwepo mwamko mkubwa wa ushiriki wa makundi ya wanawake na vijana katika
jitihada za ukuaji wa uchumi Barani Afrika hasa kupitia Sekta ya Biashara.
Aidha amesema kwamba Mkutano na
Maonesho ya Biashara yaliyofanyika yametoa elimu kubwa na kutengeneza fursa
pana kwa washiriki hao kubadilishana uzoefu na taarifa muhimu za kibiashara na
kuwataka kuendelea kubadilisha uzoefu ili kuzitumia vyema fursa za kibiashara
zilizopo katika soko huru la Afrika.
Amesema mkutano huo pia umetoa
fursa ya kuwepo mjadala maalum na kutoa mapendekezo kuhusu itifaki ya Wanawake na Vijana katika
Biashara chini ya Mkataba wa Eneo Huru la Biashara la Afrika.
Amefahamisha kuwa maoni na
mapendekezo yaliyotolewa yatazingatiwa katika uandaaji wa Itifaki hiyo ili
iweze kusaidia kuongeza ushiriki na mchango mkubwa zaidi wa Wanawake na Vijana
kwenye biashara kwa kutumia ipasavyo fursa zitokanazo na Mkataba wa Eneo Huru
la Biashara la Afrika.
Naye Waziri wa Maendeleo ya Jamii,
Jinsia wazee na Watoto Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma, amesema kwamba sera za
kiuchumi na biashara zinazotungwa na serikali za Afrika hivi sasa zinajielekez
zaidi kuunga mkono jitihada za ushiriki mpana wa wanawake na vijana katika
kukuza uchumi kupitia shughuli za kibishara.
Kwa Upande wake waziri wa Biashara
na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Omar Said Shaaban, amesema kwamba changamoto
kubwa iliyopo katika sekta ya biashara kwa vijana wa Afrika sio sera na sharia bali ni namna ya
kuzitafsiri katika kuchangia kuimarisha biashara na kuendeleza ukuaji wa uchumi
na maendeleo.
Naye Katibu Mtendaji wa Sekretariet
wa Eneo Huru la Biashara Afrika Bwana Mamkele Mene, amesema kwamba mkutano huo
uliofanyika kwa ufanisi ni muhimu kwa kuwa mjadala wake utasaidia sana katika
kupatikana suluhisho la changamotio mbali mbali za kibiashara zinazojitokeza
katika nchi za Afrika.
Imetolewa Ofisi ya Makamu wa Kwanza
wa Rais wa Zanzibar kupitia Kitengo cha Habari leo tarehe 14.09.22.
No comments:
Post a Comment