Habari za Punde

Maafisa Habari na Mawasiliano wa Wizara Wapata Mafunzo

Mhariri Mtendaji Shirika la Magazeti ya Serikali Ali Mwadini akiwasilisha mada kuhusu  Mafanikio ya Serikali kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Maafisa Habari na Mawasiliano wa Wizara mbalimbali za Serikali huko Ukumbi wa Studio Rahaleo Zanzibar
Mhariri Mtendaji wa Shirika la Magazeti ya Serikali Ali Mwadini akionyesha mfano wa kijarida maalum cha Serikali “Neema Zetu” kitakachotolewa na Shirika la Magazeti chini  ya Wizara ya Habari    kinachoelezea utendaji wa Serikali ,  wakati akiwasilisha mada ya mafanikio ya Serikali kupitia vyombo vya Habari na mitandao ya kijamii katika mafunzo ya  kuwajengea uwezo Maafisa Habari na Mawasiliano wa Wizara mbalimbali za Serikali huko Ukumbi wa Studio Rahaleo Zanzibar.
Maafisa Habari na Mawasiliano wa Wizara mbalimbali za Serikali wakifuatilia mafunzo ya kuwajengea uwezo , yaliyoandaliwa na Idara ya Habari Maelezo Zanzibar katika Ukumbi wa Studio Rahaleo.
Afisa Mawasiliano Wizara ya Nchi (OR) Fedha na Mipango  Asha Saleh akichangia mada wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Maafisa Habari na Mawasiliano  wa Wizara mbalimbali za Serikali   huko Ukumbi wa Studio Rahaleo Zanzibar, mafunzo hayo yameandaliwa na Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.
Afisa Mawasiliano Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi  Kassim Abdi  akichangia mada wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Maafisa Habari na Mawasiliano  wa Wizara mbalimbali za Serikali   yaliyofanyika katika  Ukumbi wa Studio Rahaleo, mafunzo hayo yameandaliwa na Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.
Afisa Mawasiliano Ikulu Mwatima Rashid  Issa akichangia mada wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo  Maafisa Habari na Mawasiliano wa Wizara mbalimbali za Serikali yaliyoandaliwa na Idara ya Habari Maelezo Zanzibar huko Ukumbi wa Studio Rahaleo Zanzibar.
Afisa Utumishi  Wizara ya Nchi, (OR) Katiba,Sheria, Utumishi na Utawala Bora Bakari Khamis Muhidini akiwasilisha mada kuhusu Muundo wa Utumishi wa Kada ya  Maafisa Habari na Mawasiliano wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo Maafisa Habari na Mawasiliano wa Wizara mbalimbali za Serikali  huko Ukumbi wa studio Rahaleo Zanzibar.
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.