Habari za Punde

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Lela Mussa Azungumza na Wanafunzi Wanaokwenda Nje ya Nchi kwa Mafunzo

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Lela Muhammed Mussa akisisitiza jambo wakati akizungumza Wanafunzi wa Skuli ya Kilimo wanaokwenda Nchini Israel kwa Mafunzo ya utarajal(internship) ya Kilimo na Mifugo,mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Elimu Mazizini Wilaya ya Magharibi "B" Unguja.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Lela Muhammed Mussa akizungumza na Wanafunzi wa Skuli ya Kilimo wanaokwenda Nchini Israel kwa Mafunzo ya utarajal(internship) ya Kilimo na Mifugo,mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Elimu Mazizini Wilaya ya Magharibi "B" Unguja.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Lela Muhammed Mussa amesema Serikali inatumia kila mbinu ili kuhakikisha inazalisha wataalam wazalendo nchini.

Amesema hayo wakati akiwaaga Wanafunzi kutoka Skuli ya Kilimo wanaoelekea nchini Israel kwa Mafunzo ya utarajal(internship) wa Kilimo na mifugo Katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo Mazizini Unguja.
Aamewasisitiza Wanafunzi hao kuhakikisha wanatimiza lengo linalowapeleka nchini Israel kwani Taifa linategemea mazuri kutoka kwao.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Waziri wa Wizara hiyo Mhe Ali Abdulgulam Hussein amewasisitiza Wanafunzi hao kusimamia Mila silka na utamaduni wa nchi yao kwani nayo ni tiketi ya kufanya vizuri Katika masomo yao.
Kwa upande wao Wanafunzi hao wameipongeza Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa na mahusiano mazuri na nchi nyengine hali inayopelekea vijana kujenga weledi na ujuzi kupitia nchi zilizoendelea kwa lengo la kuanzisha wataalam wazalendo.
Jumla ya wanafunzi 23 wanategemea kuondoka nchini kuelekea nchini Israel.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.