Habari za Punde

Zicco wakutana kupanga mikakati ya kupiga hatua kimaendeleo

Mkurugenzi Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Hassan Khatib Hassan akizungumza na Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali wakati wa mkutano wa Maafisa hao uliofanyika katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar. PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR

Katibu wa Jumuiya ya Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali (ZICOO ) Makame Khamis Moh’d akitoa maelezo mafupi kuhusiana na Jumuiya hiyo wakati wakijadiliana juu ya hatua waliofikia ya  kuainziasha umoja huo ,huko Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar. PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR

 

Mwenyekiti wa Jumuiya ya  Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali (ZICOO) Raya Hamad akimkabidhi cheti maalum cha usajili mlezi wa Jumuiya hiyo  Mkurugenzi wa Idara  ya Habari Maelezo Hassan Katibu Hassan  wakati wa mkutano wa Maafisa hao uliofanyika  Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar. PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR
Afisa Mahusiano Mamlaka ya viwanja wa ndege Zanzibar Mulhat Yussuf said  akichangia mada  wakati wa majadiliano katika mkutano wa Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali uliofanyika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar. PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR
Afisa Habari Wizara ya   kilimo Asha Mohammed Abdul -kadir akichangia mada wakati wa majadiliano katika mkutano wa Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali uliofanyika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar. PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR

Afisa Habari Mkoa wa Kaskazini Unguja Habibu Othman  akchangia mada  wakati wa mkutano wa Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali uliofanyika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar. PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR

 

Afisa Habari Makao Makuu ya Polisi Zanzibar Omar Hassan akichangia mada  wakati wa majadiliano ya mkutano wa Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali uliofanyika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar. PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR

Mwenyekiti wa Jumuiya ya  Maafisa Habari na Mawasiliano wa Serikali (ZICOO) Raya Hamad akizungumza na Maafisa hao wakati wa mkutano wakujadili utendaji kazi katika Jumuiya yao Uliofanyika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR


Na Bahati Habibu       Maelezo     30/9/2022

 

Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Hassan Khatibu Hassan ametoa wito kwa Viongozi wa Serikali kutambua umuhimu na majukumu ya Maafisa Habari na Mawasiliano katika sehemu zao za kazi.

 

Wito huo ameutoa wakati akizungumza na    Maafisa wa Habari na Mawasiliano wa Serikali  katika ukumbi wa Sanaa ulipo Raha leo mjini Zanzibar wa kujadili hatua waliyofikia ya uanzishwaji wa  Jumuiya ya Maafisa Habari wa Serikali Zanzibar (ZICOO).

 

Amesema kukamilika kwa usajili wa jumuiya hiyo kutasaidia viongozi wa taasisi kufahamu majukumu ya maafisa hao pamoja na kuzitatua changamoto zinazowakabili.

 

“Changamoto ziko nyingi na tutajitahidi kukabiliana nazo ili kuhakikisha maafisa wa habari wasimamia majukumu yao ya kuielezea jamii kuhusu utendaji kazi wa taasisi zao " Alisema Mkurugenzi huyo.

 

Nae katibu wa jumuiya hiyo Makame Khamis Mohamed amesema kuanzishwa kwa jumuiya kutasaidia maafisa wa habari kupata sehemu ya kufikisha changamoto zao na kuchukuliwa hatua zinazostahiki.

 

Aidha amelezea kuwa jumuiya hiyo itakuwa inawapongeza Maafisa habari wanaofanya vizuri pamoja na kutoa mafunzo kwa maafisa hao ili kuhamasisha utendaji kazi.

 

Nae Mwenyekiti wa jumuiya hiyo Raya Hamadi wakati akifunga kikao hicho ameishukuru Idara  ya Habari Maelezo kwa kuamua kuwaweka pamoja Maafisa wa habari na Mawasiliano wa taasisi za serikali kwa kuanzisha jumuiya hiyo hatua ambayo itapelekea kuimarika kwa sekta ya habari nchini.

 

Amesema hatua hiyo itapelekea maafisa hao kuzitangaza Taasisi zao ili ziweze kufikia malengo  yaliyokusudiwa na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar 

 

Nao washiriki wa mkutano huo wameshukuru  kwa kuanzishwa jumuiya hiyo hali itakayosaidia kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.