Habari za Punde

Ligoneko Atetea Ubingwa Wake Baiskeli Wanaume

Washiriki wa mbio za Km 40 kwa wanaume wakichuana katika mbio hizo Oktoba 9, 2022 ikiwa ni muendelezo wa michezo ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) inayoendelea jijini Tanga.

Bingwa mtetezi wa mbio za baiskeli kwa wanaume Omar Ligoneko wa Bohari ya Dawa nchini (MSD) akimalizia mbio za Km 40 kwa wanaume Oktoba 9, 2022 katika Uwanja wa Mkwakwani ikiwa ni muendelezo wa michezo ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) inayoendelea jijini hapa.

Mshindi wa kwanza mbio za baiskeli kwa wanawake Alavuya Ntalima wa Wizara ya Mambo ya Ndani akimalizia mbio za Km 25 kwa wanawake Oktoba 9, 2022 katika Uwanja wa Mkwakwani ikiwa ni muendelezo wa michezo ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) inayoendelea jijini Tanga.





Na Mwandishi Wetu, Tanga

Wakati bingwa mtetezi wa mbio za baiskeli kwa wanaume Omar Ligoneko wa Bohari ya Dawa nchini (MSD) ametetea kiti chake, mchezaji Scolastica Hasiri wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) ameshindwa kutetea ubingwa wake kwa kushika nafasi ya pili katika michezo ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) inayoendelea jijini hapa.

Ligoneko ambaye ni bingwa mtetezi mara mbili mfululizo kwa upande wa wanaume aliwashinda wengine 19 baada ya kumaliza mbio hizo za Km 40 akitumia muda wa saa 2:46.00; akifuatiwa kwa karibu na Steve Sanga wa Wizara ya Afya aliyemaliza kwa saa 2:46.20 na watatu ni Silaji Mohamed wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi aliyetumia muda was aa 2:49.

Kwa upande wa wanawake imedhihirisha ule usemi unaosema “usikate tamaa mambo mazuri yanakuja”, haya yamejidhihirisha kwa Alavuya Ntalima wa Wizara ya Mambo ya Ndani baada ya kutwaa ubingwa kwa mara ya kwanza baada ya kushiriki kwenye michezo hii takribani miaka mitano nyuma, lakini amekuwa akishika nafasi ya tano na kuendelea.

Alavuya aliyewashinda wanawake wengine watano akitumia muda wa saa 1:58, akifuatiwa na Scolastica aliyetumia saa 1:59 na Bertha Wilson wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) akitumia saa 2:03.

Wakizungumzia ubingwa wao Ligoneko amesema amepata changamoto ya ushindani kwa mashindano haya kushirikisha vijana zaidi, tofauti na yeye anayekaribia kutimiza miaka 50; huku Navuya amesema kuwa alijiandaa vyema kutwaa ubingwa kutokana na kushiriki mara nyingi michezo hii na ile ya Mei Mosi kila mwaka lakini hakuwahi kutwaa ubingwa zaidi ya kushika nafasi ya katikati.

Naye Alavuya ametwaa ubingwa wa wanawake katika mbio za Km 25 kwa mara ya kwanza tangu aanze kushiriki michezo hiyo takribani miaka mitano iliyopita katika mashindano hayo.

Mchezo wa mbio za Baiskeli kwa upande wa wanawake ulianza majira ya saa 1:00 asubuhi katika eneo la Mkanyageni ambao walienda umbali wa KM 25 wakati mbio hizo kwa upande wa wanaume zilianza majira ya saa 1:40 katika ene la Kibada wilaya Mheza mkoani Tanga ambao wao walienda umbali wa KM 40.

Aidha, katika mchezo wa riadha wanaume katika mbio za M 800 mshindi wa kwanza ni Elibariki Buko kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, mshindi wa pili ni Eliud Kitwika kutoka Wizara ya Mifugo Uvuvi wakati mshindi wa tatu ni Ramadhani Mwakilongo kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi).

Mshindi wa kwanza mbio hizo za M 800 kwa wanawake ni Scholarstica Hamis kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi), mshindi wa pili ni Nyamwiza Ndibalema kutoka Wizara ya Madini na mshindi wa tatu ni Furaha Kaboneka kutoka Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi.

Katika mbio za M 3000 mshindi wa kwanza ni Elibariki Buko kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, mshindi wa pili ni Joseph Kachali kutoka Wizara ya Afya wakati mshindi wa tatu ni Anangisye Mwangoka kutoka Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) wakati kwa upande wa wanawake mshindi wa kwanza ni Justa George kutoka Idara ya Mahakama, mshindi wa pili ni Nyamwiza Ndibalema kutoka Wizara ya  Madini na mshindi wa tatu ni Secilia Msuma kutoka Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Wakati huo huo mchezo wa kurusha tufe wanaume na wanawake pia ulichezwa katika uwanja shule ya Sekondari ya Ufundi Tanga ambapo mshindi wa kwanza kwa upande wa wanaume ni Alinanuswe Mwakiluma kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (sekta ya Ujenzi), mshindi wa pili ni Said Mmbaga kutoka Wizara ya Maji, mshindi wa tatu ni Cassian Luoga kutoka Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi. Kwa upande wa wanawake katika mchezo huo mshindi wa kwanza ni Akanganyila Theophil kutoka Idara ya Mahakama, mshindi wa pili ni Enid Geofrey kutoka Tume ya Walimu Tanzania (TSC).     

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.