Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi Ameshuhudia Utiaji wa Saini wa Ushirikiano Kati ya Zanzibar na Oman

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi,  akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake nchini Oman, alishuhudia utiaji saini wa hati za ushirikiano baina ya Zanzibar na Oman. 

Hati hizo zinahusu masuala ya Miundo Mbinu ya TEHAMA, ambapo Waziri wa Ujenzi.Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Mhe.Dk.Khalid Salum Mohammed, ametia saini kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi  Zanzibar. 

Hati nyingine ilikuwa inahusu ni Elimu ya Juu, ambapo Waziri wa Nchi Ofizi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Mhe.Dk. Saada Mkuya Salum ametia saini kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,  ambapo hati zinazohusu mpango wa utekelezaji wa hati za ushirikiano kuhusu utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka ambao umesainiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Utalii Zanzibar. Bi.-Fatma Mbarouk Khamis. 

Hati nyingine za ushirikiano zilihusu Urithi na Mambo ya Kale ambapo Dk. Saada Mkuya Salum ametia saini na kumalizia na  hati ya  Ushirikiano inayohusu uwekaji Mifumo ya Mapato ya Kidijitali. 


 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.