Habari za Punde

Walimu wa Kidato cha tano na cha sita wapongezwa

 Na Khadija Khamis –Maelezo 01/10/2022.

Mkuu wa Wilaya ya Mjini Rashid Simai Msaraka ametoa pongezi kwa walimu  kwa juhudi zao walizozichukuwa kwa kufanikisha matokeo mazuri kwa wanafunzi wao


Akitoa pongezi hizo kwa walimu wa kidatu cha tano na cha sita  wa Wilaya ya Mjini katika ukumbi wa skuli ya Sekondari Lumumba wakati wa kupewa vyeti pamoja na tafrija fupi .


Amesema walimu wamefanya kazi kubwa ya kuhakikisha wanafunzi wao wanazifikia ndoto zao jambo ambalo limewatia moyo viongozi na wazazi wao kiujumla ,


Aidha alisema serikali ya Mkoa pamoja na Wilaya  inawapongeza walimu wa wilaya ya mjini kwa kufaulisha wanafunzi wengi kwa kiwango cha daraja la kwanza wa kidatu cha sita .


alieleza kuwa jumla ya wanafunzi 519  wa kidatu cha sita waliofaulu katika daraja ya kwanzo kwa Mkoa Mjini Magharibi mwaka 2022 kati ya hao wanafunzi 257 kutoka Wilaya ya Mjini,  jambo ambalo limewapatia nafasi ya Kwanza kwa kupasisha wanafunzi wengi kulingana na wilaya nyengine za Zanzibar  .


Mkuu huyo aliwataka walimu hao kushirikiana kwa pamoja katika changamoto mbali mbali zitakazojitokeza ili kuzitatua kwa kutoa taarifa katika serikali ya mkoa na wilaya .


Nae Afisa Elimu Wilaya ya Mjini,  Mwalimu Hassan Abasi Hassan akisoma risala ya walimu hao alisema mara nyingi pongezi hutolewa kwa wanafunzi tu walimu husahauliwa kwa mara hii ni mwaka wa kwanza kupongezwa

 

Alifahamisha kuwa kwa matokeo ya mwaka huu ya kidatu cha sita ni ya kupigiwa mfano kwa uzuri wake haujawahi kutokea kwa asilmia 99.6 kulinganisha na asilimia 97.6 ya mwaka jana.


aidha alisema ongezeko la ufaulu kuanzia daraja la kwanza la pili na la tatu litazidi kuimarika kwa mashirikiano ya walImu Wanafunzi pamoja na wazazi ili kuhakikisha wanafuata kauli mbiu ya”ONGEZA UFAULU WA DARAJA LA KWANZA NA ONDOA ZERO MJINI”.


kwa upande wa Katibu Tawala Wilaya ya Mjini   Dkt Saidi Haji Mrisho amewataka walimu kuendelea kuchapa kazi kwa kutumia mbinu mbali mbali za ustadi ili lengo la ufaulu la daraja la kwanza lifanikiwe na kuepuka zero kufuta daraja la nne.  


Aidha alisema juhudi hizo zitamjengea imani kubwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Husein Ali Hassan Mwinyi kwa jitihada zake za kimarisha miundombinu mbali mbali kwa walimu na wanafunzi yenye lengo la kuimarisha kiwango cha  ufaulu chini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.