Habari za Punde

Kampeni ya mzunguko wa nne wa chanjo ya Polio Surua kuanza kesho

 Na Khadija Khamis -Maelezo.16/11/2022.


Jamii imetakiwa kushiriki kikamilifu katika zoezi la Kampeni ya mzunguko wa nne wa chanjo  ya polio Surua na vitaman  A.ambayo inatarajiwa kuanza tarehe 17 hadi 20 mwezi huu.

Akitoa kauli hiyo Afisa wa Afya Wilaya ya Mjini Faki  Makame Faki katika ukumbi wa Afisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Amani amesema Chanjo ni kinga kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano ambao huwa kinga zao za mwili  ni mdogo na ni rahisi kupata maambikizo ya maradhi mbalimbali

 Amesema kwa kuwapatia chanjo watoto hao kutasaidia kuwakinga na maradhi ya kuambukiza hivyo Iko haja ya jamii kuelewa na kuitumia fursa hiyo kwa kuhakikisha watoto wao wanashiriki katika zoezi hilo

Aidha amesema kuwa magonjwa ya Polio na Surua ni mabaya Sana kwani husababisha kupata ulemavu wa kudumu kwa kupoteza viungo kupofua kupata uziwi na hata kupelekea kupoteza maisha.

Nae Mratibu wa Elimu ya Afya Riski Mohamed Sleiman amesema kumekuwa na changamoto ya Surua katika Wilaya nne kwa Unguja, ikiwemo na Wilaya ya Mjini ambayo imeshukiwa na Kesi 218 za ugonjwa huo

Alifahamisha kuwa kwa Zanzibar kumeshukiwa kesi 1662 za Surua na vifo vinane vimeripotiwa kutoka Magharibi A na B.

Akitoa wito kwa Jamii kuwataka kutoa mashirikiano ya pamoja katika kufanikisha zoezi hilo Ili kuwakinga watoto na maambukizo ya maradhi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.