Habari za Punde

Mhe Hemed aufungua Mkutano wa Kumi na Sita wa Taasisi zinazosimamia udhibiti wa Nishati Afrika

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla akizungumza na washiriki wa Mkutano wa Kumi na Sita wa Taasisi zinazosimamia udhibiti wa Nishati Afrika uliofanyika Ukumbi wa Madinat Al Bahr Mbweni Zanzibar alipohudhuria kufungua Mkutano huo.
Waziri wa Maji, Nishati na Madini Mhe. Shaaban Ali Othman akieleza machache katika Mkutano wa Kumi na Sita wa Umoja wa Taasisi zinazosimamia udhibiti wa Nishati Afrika uliofanyika Ukumbi wa Madinat Al Bahri Mbweni Zanzibar.
 Mwenykiti wa Umoja wa Taasisi zinazosimamia udhibiti wa Nishati Afrika Bwana Balthazar Nganikiye akizungumza malengo ya Mkutano wa Kumi na Sita wa Umoja huo  unaofanyika Ukumbi wa Madinat Al Bahr.
Washiriki kutoka Nchi mbali mbali Afrika waliohudhuria Mkutano wa Kumi na Sita wa Umoja wa Taasisi za udhibiti wa Nishati A Afrika  uliofanyika Ukumbi wa Madinat Al Bahr.

Na Abdulrahim Khamis

Mashirikiano ya Pamoja yanahitajika kukuza Sekta ya Nishati ya Maji  kwa Nchi za Afrika ili kuboresha huduma hizo kwa Wananchi wa Nchi hizo.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ametoa kauli hiyo katika Mkutano wa Kumi na Sita wa kujadili masuala ya Nishati kwa Nchi za Afrika uliofanyika Hotel ya Madinat Al Bahri Mbweni jijini Zanzibar.

Ameeleza kufurahishwa kwake kuona Mkutano huo unazindua Ripoti ya ugawaji wa Maji barani Afrika ambao itatoa Muhtasari wa hali ya udhibiti wa utoaji wa huduma hizo.

Mhe. Hemed ameeleza kuwa kuwepo kwa ripoti hiyo kutaweza kutoa Fursa kwa Zanzibar na  Nchi nyengine kupata uzoefu kwa Nchi mbali mbali jinsi ya udhibiti wa Huduma ya Maji wanavyofanyakazi na namna wanavyokabiliana na Changamoto wanazokumbana nazo katika udhibiti huduma hiyo.

Aidha meeleza kuwa Mkutano huo utatoa Fursa kwa Washirika wa Ndani na Nje ya Nchi kuwa na mtazamo wa pamoja wenye lengo la kubadilishana mawazo na uzoefu katika mifumo ya udhibiti wa maji safi.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ameeleza kuwa Nchi zote Duniani zinapambana na kufikia malengo ya Dunia ya maendeleo hasa upatikanaji wa Huduma ya Maji Safi kwa wote hivyo ni wajibu Kwa Taasisi za udhibiti Huduma hiyo kusimamia ipasavyo Sekta husika ili kufikia malengo hayo ya Dunia.

Mhe. Hemed ameipongeza Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati Zanzibar (ZURA) kwa namna wanavyosimamia sekta hiyo na kueleza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuwajengea uwezo watendaji wa Mamlaka hiyo pamoja na kukuza ushirikiano uliopo na Taasisi nyengine.

Sambamba na hayo Mhe. Hemed ametumia Fursa hiyo kuwakaribisha  washiriki hao kuwekeza Zanzibar katika sekta mbali mbali hasa Sekta ya Mafuta na Gesi na Sekta nyengine mbali mbali.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Taasisi zinazodhibiti Huduma za Nishati Afrika Bwana Balthazar Nganikiye ameeleza kuwa Lengo la kuwepo kwa Mkutano huo ni kuzijengea uwezo Mamlaka za Udhibiti wa Nishati Nchi za Afrika pamoja na kukuza mashirikiano kwa Nchi hizo.

Aidha amesema Umoja huo una jukumu la kujua Changamoto zinazozikabiliana Nchi za Afrika katika usambazaji wa Maji na kujadili njia bora ya kutatua changamoto hizo.

Nae Naibu Waziri wa Maji, Nishati na Madini Mhe. Shaaban Ali Othman amesema Mkutano huo kufanyika Zanzibar utatoa Fursa kujua Njia nzuri zinazotumiwa na Nchi za Afrika hasa katika suala la usambazaji wa Maji jambo ambalo litasaidia Serikali kuwafikishia Wananchi wake huduma hiyo.

Mkutano huo wa Kumi na Sita uliowakutanisha washiriki zaidi ya Nchi Hamsini za Afrika ni mara ya kwanza kufanya hapa Zanzibar.

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.