Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman akisalimiana na baadhi ya Viongozi wa Madrasat Hayaatul Atfaal ya Baghani Wete Pemba wakati alipowasil katika ukumbi wa Banquate Kiembe Samaki wilaya ya Magharib B Unguja kwa ajili ya ufunguzi wa Mkutano wa Tano wa mwaka wa Madrasat Hayaatul Atfaal ya Baghani Wete Pemba iliofanyika 25.12.2022.
Baadhi ya wanafunzi Waliohudhuria katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Madrasat Liaatfal ya Baghani Wete Pemba wakiwa katika Picha ya Pamoja wakisoma dua ya Kumkaribisha Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman alipowasili ili kuufungua rasmi mkutano huo huko katika ukumbi wa Banquate Kiembe Samaki wilaya ya Magharib B Unguja leo tarehe 25.12.2022. Picha na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Kitengo cha habari.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman akipokea zawadi kutoka mmoja wa Viongozi wa Madrasat Hayaatul Atfaal ya Baghani wete Pemba wakati Mhe. Othman alipowasil katika ukumbi wa Banquate Kiembe Samaki wilaya ya Magharib B Unguja ili kufungua Mkutano wa Tano wa mwaka wa Madrasa hiyo leo tarehe 25.12.2022. Picha na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Kitengo cha habari.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Alhaj Othman Masoud Othman akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Washiriki na Viongozi mbali mbali waliohudhuria Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Madrasat Liaatfal ya Baghani Wete Pemba baada ya kumalizika kwa ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Banquate Kiembe Samaki wilaya ya Magharib B Unguja
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman akifungua Mkutano wa Tano wa mwaka wa Madrasat Hayaatul Atfaal ya Baghani Wete Pemba uliofanyika Katika ukumbi wa Banquate Kiembe Samaki wilaya ya Magharib B Unguja 25.12.2022.
Na.OMKR.
MAKAMU wa Kwanza wa Rais wa
Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, amesema Zanzibar imekabiliwa na janga kubwa
la kimaadili na kusababisha kuwepo baadhi ya watumishi wasomi wanaofanya vitendo
vya kuiibia nchi mamilioni ya fedha
kupitia dhamana zao za kazi.
Mhe. Othman ameyasema hayo huko
Kiembesamaki Wilaya ya Magharib Unguja katika ukumbi wa Banquate alipofungua Mkutano Mkuu wa tano wa mwaka
wa Madrsat hayaatul atfaal ya Baghani Wete Pemba.
Mhe. Othman amsema watu wanaofanya
vitendo vya kuiba mali za serikali sio wale walioishia darasa dogo la elimu
lakini wengi wao ni wasomi wenye mashahada ya juu na wanafanya hivyo kutokana
na kutokana wazee kutokuwa na maadili mema yanayotokana na muongozo wa dini.
Ameitaka jamii kuhakikisha kwamba
wanawaandaa vijana katika maadili kwa kuwafundisha tabia njema za kumcha
mwenyezimungu muumba ili waweze kuwa watu wema ndani ya nchi yao.
Amefahamisha kwamba jukumu la
malezi bora yenye maadili ni wajibu wa
wazazi wenyewe na Kwamba sio busara jambo hilo kuachwa kwa walimu pekee ama
kuonekana kwamba ni jukumu la serikali zaidi badala ya wazazi na jamii kwa jumla.
Ameitaka jamii kuwekeza katika
kukifanya kizazi kisiihame kuraani na maamuru yake kwa kufanya hivyo ni kuiepusha jamii na taifa
kwa jumla katika maafa makubwa ya kufanya mitendo viovu.
Amefahamisha kwamba Zanzibar
inahistoria kubwa katika kufuata mila na tabiaa njema zinazotokana na muongozo
wa dini na kwamba bila jamii kujitahidi kwaelea vyema vijana upo uwezekano wa
ladha na harufu njema ya kimaadili ya Zanzibar kupotea.
Hata hivyo ameupongeza uongozi wa
Madrasa hiyo kwa jitihada kubwa za kuwalea
watoto kupitia misingi ya quran pamoja na kuwa na utaratibu mzuri wa
kusimamia madrasa hiyo jambo ambalo linakosekana katika taasisi nyingi za namna
hiyo hapa Zanzibar.
Naye Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar
Sheikh Othman Ame Chum akimkaribisha Mhe. Othman kufungua Mkutano huo amesema
kwamba Zanzibar inavipaji vingi vya
watoto na kwamba walimu waendelea na kazi kubwa ya kuvilea na kuvikuza vipaji
hivyo.
Amesema changamoto ya ukosefu wa
maadili iliyopo Zaanzibar kwa vijana kuyjiingiza kwenyer vitendo viovu kama
vile vya utumiaji wa madawa ya kulevya , udhalilishaji dawa yake sio kuwepo
sharia kali pekee bali ni pamoja na kuwajenga watoto na jamii kwa jumla katika
maadili mema.
Akisoma Risala hiyo mbele ya Mgeni
rasm Maalim Rashid Sinan alimema kwamba
pamoja na madras kutoa masheikh na waaalimu kadhaa lakini imekabiliwa na
changamoto mbali ikiwemo vikalio, vifaa vya kufundishia kwa mfumo wa kisasa na
kwamba waislamu ni muhimu kujitolea kusaidia madrasa ili dini ya kiislamu iweze
kusonga mbele.
Imetolewa na ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kupitia kitengo chake ha Habari leo tarehe 25.12.2022.
No comments:
Post a Comment