Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Mwinyi Ametoa Mkono wa Pole kwa Familia ya Marehemu Zainab Esmail Alloo Kiponda

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Alhaj. Dk.Hussein Ali Mwinyi akitowa mkono wa pole kwa familia ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Bi.Yasmin Alloo nyumbani kwao Kiponda Wilaya ya Mjini Unguja kwa kufiliwa na shangazi yake Marehemu Zainab Esmail Hasham Alloo, mwanzoni  mwa mwezi huu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na familia ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Bi.Yasmin Alloo wakiitikia dua inayosomwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi (kushoto) alipofika kutowa mkono wa pole kwa Familia ya Marehemu Zainab Esmail Alloh  nyumbani kwao Kiponda 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Alhaj.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Bi.Yasmin Alloo baada ya kumfariji nyumbani kwake Kiponda kwa kufiliwa na shangazi yake BI.Zainab Esmail Hasham Alloo, aliyefariki mwanzoni  mwa mwezi huu.[Picha na Ikulu] 23/12/2022.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.