Habari za Punde

Ahukumiwa Miaka 30 kwa Kosa la Kulawati

Na Masanja Mabula PEMBA

KIJANA Fadhili Musa Sharif 35 mkaazi wa Kifumbikai Wete amehukumiwa  na Mahakama maalum ya kupambana na makosa ya udhalilishaji Mkoa wa Kaskazini Pemba kutumikia chuo Cha mafunzo miaka 30 kwa kosa la kumlawiti mvulana mwenye umri wa miaka 15

Hukumu hiyo imetolewa Jana na hakimu wa mahakama hiyo Mhe.Ali Abdulrahman Ali.

Imedaiwa mahakamani hapo na mwendesha mashitaka wa Serikali Juma Mussa Omar kuwa mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo tarehe 27 /7/2021 majira ya saa sita na nusu usiku huko Kifumbikai Jambo ambalo ni kosa kisheria  kinyume na kifungu Cha 115(1) Cha Sheria namba 6 ya mwaka 2018 Sheria za Zanzibar .

Kesi hiyo ilifunguliwa mahakamani hapo terehe 6/12/2022 ambapo Jumla ya mashahidi watano wametoa ushahidi wao

Awali kabla ya kusomwa hukumu hiyo upande wa mwendesha mashitaka wa Serikali uliiomba mahakama itoe adhabu  Kali kwa mshitakiwa ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.

"Naiomba mahakama itoe adhabu Kali kwa mshitakiwa kwani makosa ya aina hii yanazidi kuongezeka na hii itakuwa fundisho kwake na wengine wenye tabia kama hii"alisema.

Akisoma hukumu hakimu Mhe.Ali Abdulrahman Ali amesema mahakama imeridhika na ushahidi ulitolewa na kumwamuru aende kutumikia chuo Cha mafunzo miaka 30 pamoja na kumlipa mwathirika shilingi milioni moja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.