Habari za Punde

Mhe Hemed ajumuika na waumini katika Sala ya Ijumaa Masjid Jumaa Mwera Pongwe


 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla akisalimiana na Waumini wa Masjid JUMAA uliopo Mwera Pongwe  Wilaya ya Kati mara baada ya kumalizika Swala ya Ijumaa.

Wazazi wametakiwa kuwasimamia vyema watoto wao kupata elimu zilizo bora kwa maslahi ya familia, jamii na taifa kwa ujumla.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Alhajj Hemed Suleiman Abdulla ameyasema  hayo  wakati akisalimiana na Waumini wa Masjid JUMAA uliopo Mwera Pongwe  Wilaya ya Kati mara baada ya kumalizika Swala ya Ijumaa.

Amesema ni wajibu wa kila mzazi kuhakikisha anawasimamia vyema watoto wake kwa kuwapatia  haki yao ya msingi ya elimu iliyobora  ili kupata taifa lenye wasomi wengi na wenye kuweza kutatua matatizo  yanayoweza kujitokeza baina yao.

Mhe. Hemed amesema kuwa yapo mambo ambayo hufanya na watoto au vijana bila ya kujua nini anafanya na nini athari yake hapo baadae hivyo pindipo wazazi watakapo wapatia watoto wao elimu iliyobora itasaidia kuondosha yale matendo yote maovu ambayo hufanya na vijana  ikiwemo utumiaji wa madawa ya kulevya, wizi, udhalilishaji na mengineyo.

 

Aidha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amewasisitiza wazizi kulisimamia vyema suala la elimu kwa watoto wao kama ilivyoamrishwa katika kitabu kitukufu cha Qur'an kwamba kila mmoja ana haki ya kutafuta elimu ndani na nje ya nchi kwa maslahi ya jamii  na taifa kwa ujumla.

Sambamaba na hayo Alhaji Hemed amewataka waumini na wananchi kwa ujumla kuendelea kuiombea dua nchi yetu pamoja na kumuombea dua rais wa zanzibar na mwenyekiti wa barazaa la mapinduzi Alhajji Dkt. Hussein Ali Mwinyi ili aweze kuyasimamia na kuyatekeleza yale yote aliyoyakusudia ya kimaendeleo kwa maslahi ya wazanzibari na watanzania kwa ujumla.

 

Kwa upande Maalim SAID KHALFAN katika Khutba ya Sala ya Ijumaa  amewataka waumini kudumisha mapenzi baina yao ili kupata radhi za Allah hapa duniani na kesho Akhera na kuachana na yele yote ambayo humkirihisha mwenyezi mungu mtukufu.

Amesema uislamu unasisitiza sana mapenzi baina ya waislamu na unakataza sana waislamu kuchunguzana na kuchukiana kwani kufanya hivyo kunaondosha mapenzi baina yao na kusababisha kukosa radhi za Allah S.W.

……………………………

Ali Muhamed

Afisi ya makamu wa pili wa rais

06/01/2023

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.