Na Maulid Yussuf WMJJWW
Wilaya ya Kaskazini A.
Mwakilishi wa Viti Maaluumu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe Riziki Pembe Juma ambae pia ni Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto amewataka wazazi kuwafuatilia kwa karibu watoto wao ili kuwaepusha na vitendo vya udhalilishaji nchini.
Mhe Riziki ameyasema hayo wakati alipokabidhi matofali pamoja na Saruji kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa jengo la ofisi ya UWT Wilaya Kaskazini A Unguja.
Amesema hivi sasa vitendo vya udhalilishaji vimekuwa vikiharibu taswira ya nchi ambapo hivi sasa wafanyaji wa vitendo wamegeuka kuwaharibu zaidi watoto wa kiume.
Hivyo amewaomba wazazi kushirikiana na kusaidiana katika kuwalinda watoto kwani athari ya matendo hayo ni kubwa kwa famila na Taifa kwa ujumla.
Aidha Mhe.Riziki amewataka wanachama wa Umoja wa Wanawake Tanzania UWT Mkoa wa Kaskazini Unguja kuhakikisha wanaongeza idadi ya wanachama katika umoja wao ili kuimarisha umoja huo.
Amesema katika kuadhimisha miaka 46 ya Chama cha Mapinduzi ni vyema UWT kushirikiana katika kuhakikisha wanachama wa chama hicho wanajiunga na umoja huo.
"Katika Mkoa wetu ni lazima tuhakikishe nambari inaongezeka kwa wanachama kama chama kinavyozidi nambari kwan mwaka jana ilikuwa 45 mwaka huu 46 basi na wanachama lazima wazidi." Amesisitiza Mhe.Riziki.
Akizungumzia kuhusu kumaliza ujenzi wa ofisi za UWT Wilaya ya Kaskazini A. Mhe Riziki amesema ni vyema kufanya tahmini ya mahitaji ya vitu vinavyohitajika ili kuzungumza na viongozi wengine katika kusaidia ujenzi huo.
Hata hvyo amesema wanachama nao wana nafasi ya kuchangia maendeleo ya ujenzi huo, hivyo ni vyema kushirikiana kila mmoja katika kutoa mchango wake ili kumaliza ujenzi huo.
Nae Mwenyekiti wa UWT Wilaya Kaskazini A Unguja bi Lucy John Mpembo, amemshkuru Mhe Riziki kwa uamuzi alioutoa katika kuchangia ujenzi wa jengo la Ofisi yao ikiwa ni miongoni mwa kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi.
Akisoma taarifa ya mradi wa UWT Wilaya ya Kaskazini A, Katibu wa Wilaya hiyo ndugu Bikungu Hamad Mohd amesema ujenzi wa ofisi wa UWT unatarajiwa kuwa na vyumba viwili kwa ajili ya ofisi za Jumuiya, chumba kimoja kwa ajili ya mlango wa biashara ya duka, ambapo mpaka hatua iliyopo sasa jumla ya shilingi milioni 9000.
Jumla ya matofali 650 pamoja na mifuko ya saruji 10 imetolewa kwa ajili ya kumalizia hatua ya ujenzi wa tofali katika ofisi hiyo.
No comments:
Post a Comment