Habari za Punde

Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan amuapisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Natu El-Maamry Mwamba na Ndugu Griffin Venance Mwakapeje, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Dkt. Natu El-Maamry Mwamba kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 09 Januari, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Ndugu Griffin Venance Mwakapeje kuwa Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 09 Januari, 2023.

 

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria Ndugu Griffin Venance Mwakapeje na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Ndugu Emmanuel Mpawe Tutuba wakila Kiapo cha Maadili kwa Viongozi, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 09 Januari, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali mara baada ya Hafla ya Uapisho iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 09 Januari, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Moses Mpogole Kusiluka, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Ndugu Emmanuel Mpawe Tutuba, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, Katibu wa Tume ya Kurekebisha Sheria Ndugu Griffin Venance Mwakapeje na Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Sivangilwa Mwangesi mara baada ya hafla ya Uapisho iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 09 Januari, 2023.
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.