Habari za Punde

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Yatoa Upimaji na Matibabu kwa Wagonjwa wa Moyo. Hospitali ya Mnazi Mmoja Unguja kwa Siku Tano Kuazia leo 23 hadi 27 Januari 2023

Daktari wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Magreth Ng’ondya akimwelekeza jinsi ya kutumia dawa za moyo Mzee Saleh Khalfan  aliyefika leo katika Hospitali ya Rufaa Mnazi Mmoja Zanzibar kwa ajili ya kupata huduma ya upimaji na matibabu ya moyo yanayofanyika katika Hospitali hiyo. JKCI kwa kushirikiana na Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar wanafanya kambi maalum ya matibabu ya moyo ya siku tano kwa watoto na watu wazima.Mfanyakazi wa Hospitali ya Rufaa Mnazi Mmoja Zanzibar Yasir Ally akimpima urefu na uzito mtoto aliyefika katika hospitali hiyo leo kwa ajili ya kupata huduma ya  upimaji na matibabu ya moyo. Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar wanafanya kambi maalum ya matibabu ya moyo ya siku tano kwa watoto na watu wazima.
Afisa Uuguzi wa Taasisi  ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)  Tumpale Kionjola akimpima shinikizo la damu mwilini (BP) mama Amina Marzuk aliyefika katika Hospitali ya Rufaa Mnazi Mmoja Zanzibar leo kwa ajili ya kupata huduma ya  upimaji na matibabu ya moyo. JKCI kwa kushirikiana na Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar wanafanyaka kambi maalum ya matibabu ya moyo ya siku tano kwa watoto na watu wazima.
Mtafiti wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Makrina Komba akimuuliza maswali mama Mwajuma Kidawa aliyefika leo katika Hospitali ya Rufaa Mnazi Mmoja Zanzibar kwa ajili ya kupata huduma ya upimaji na matibabu ya moyo yanayofanyika katika hospitali hiyo. JKCI kwa kushirikiana na Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar wanafanyaka kambi maalum ya matibabu ya moyo ya siku tano kwa watoto na watu wazima.
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.