Habari za Punde

Dimwa akagua mradi wa ujenzi wa soko la Mwanakwerekwe na Bungi

NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohammed Said Mohammed (Dimwa), akikagua ujenzi  wa masoko ya Mwanakwerekwe na Bungi Zanzibar.

Na.Is-hasa Omar. ZANZIBAR.

NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Mohammed Said Mohammed (Dimwa), ameitaka kampuni ya ujenzi iliyopewa dhamana ya kujenga Masoko ya Mwanakwerekwe na Bungi nchini kukamilisha ujenzi huo kwa wakati.

Kauli hiyo ameitoa leo katika ziara yake ya kukagua ujenzi wa miradi hiyo huko Mwanakwerekwe na Bungi Zanzibar.

Dkt.Dimwa,alisema wananchi wana matarajio makubwa juu ya miradi hiyo kwani ndio sehemu waliyokuwa wakipata kipato.

Alisema masoko ni sehemu muhimu inayowawezesha wananchi kujiajiri wenyewe.

Katika maelekezo yake Naibu Katibu Mkuu huyo Dkt.Dimwa, aliyasisitiza makampuni yanayojenga masoko hayo kukamilisha ujenzi huo kwa mujibu wa mikataba waliofunga na Serikali.

Alieleza kwamba ujenzi huo ni miongoni mwa utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020/2025 ambayo ndio mkataba halali ulifungwa baina ya Chama na Wananchi.

“Nimekuja kuangalia ujenzi wa masoko haya umefikia hatua gani ili wananchi nao wajue kuwa Chama walichokipa dhamana ya kuongoza nchini kinatekeleza kwa vitendo ahadi zake.”, alisema Dkt.Dimwa.

Naye Katibu wa Kamati maalum ya NEC,Idara ya mambo ya Siasa na uhusiano wa Kimataifa Ndg.Khadija Salum Ali,alisema CCM itaendelea kusimamia maslahi ya wananchi kwa kuwajengea miundombinu ya kisasa.

Alieleza kuwa Chama kitaendelea kufuatilia miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali ili ikamilike kwa wakati husika.

Naye Mkandarasi wa kampuni ya ujenzi ya Emirates construction Limited Mhandisi Omar Mbarouk Omar, alisema wanaendelea na kutekeleza majukumu yao kwa kasi kubwa licha kuwepo na changamoto ya umeme.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.