Habari za Punde

Mbeto atembelea waasisi wa CCM Wilaya ya Mjini na Dimani kichama

KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Ndg. Khamis Mbeto Khamis, akizungumzia masuala mbali mbali ya kiutendaji katika kipindi Maalum cha Radio Bahari FM kinachoongozwa na Mtangazaji wa Kituo hicho Donald Martin Kabemba.
KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Ndg. Khamis Mbeto Khamis,akizungumza na Watendaji wa CCM Wilaya ya Mjini kabla ya kuanza ziara yake ya kuwatembelea Wazee.
KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Ndg. Khamis Mbeto Khamis,akizungumza na muasisi wa CCM Bi.Shawali Abass Kheri nyumbani kwake Miembeni Zanzibar.
KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Ndg. Khamis Mbeto Khamis,wakiomba dua mara baada ya kuzungumza na Muasisi wa CCM Ndg. Aziz Mohammed Ibrahim nyumbani kwake Miembeni.
KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Ndg. Khamis Mbeto Khamis(kulia), akibadilisha mawazo na Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Mkoa Mjini kichama Ndg. Boraafya Silima Juma(kushoto) nyumbani Zanzibar.
KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Ndg. Khamis Mbeto Khamis(kulia), akizungumza na Waziri Mstaafu wa Wizara ya Kilimo Zanzibar Ndg. Burhan Saadat Haji(kushoto).
KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Ndg. Khamis Mbeto Khamis,akiwa na msafara wake wakitembelea Viongozi wastaafu na makada wa CCM katika Wilaya ya Mjini.

NA IS-HAKA OMAR,ZANZIBAR.
KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Ndg. Khamis Mbeto Khamis, amewasihi viongozi na watendaji wa Chama hicho kuendeleza utamaduni wa kuwatembelea Waasisi wa Chama na Serikali.


Nasaha hizo amezitoa katika ziara maalum ya kuwatembelea waasisi na viongozi wastaafu wa Chama na Serikali, katika Wilaya za Mjini na Dimani kichama.

Mbeto alieleza kuwa mtaji mkubwa wa Chama Cha Mapinduzi ni watu mbalimbali wakiwemo wastaafu katika sekta za umma na binafsi ambao ndio walioweka mazingira mazuri ya kiutendaji na kiutawala katika Serikali za sasa.

Alisema Wazee hao ni kundi muhimu katika ustawi wa Chama kisiasa kwani busara,hekima,fikra na maono yao vinachangia upatikanaji wa ushindi wa CCM.

Katika maelezo ya Katibu wa Kamati Maalum Mbeto, alisema ubobezi wa Chama Cha Mapinduzi katika masuala ya kisiasa,kijamii,kiuchumi,kimaendeleo na kiutawala vinatokana na misingi imara iliyoasisiwa na kundi hilo la wazee.

Pamoja na hayo aliwambia Viongozi hao wa zamani kweamba CCM ina thamini juhudi na mchango wao katika harakati za maendeleo nchini.

Aidha aliwaahidi kuwa katika juhudi za kuenzi na kulinda juhudi zao kwa vitendo Chama kitaendelea kutekeleza maelekezo ya ibara ya tano(5) ya Katiba ya CCM ya mwaka 1977 toleo la mwaka 2022 kwa kuhakikisha Chama kinashinda kwa kila uchaguzi wa Dola.

Aliwaomba Wazee hao kutoa ushauri wao pale wanapoona kuwa changamoto za kiutendaji ndani ya Chama Cha Mapinduzi katika Serikali zake mbili ya Zanzibar na Jamhuri kwa ujumla.

“Wazee wetu nitumie nafasi hii kukupongezeni kwa utendaji wetu mzuri mlioitumikia serikali na Chama kwani misingi mliyoiweka nyinyi ndio leo hii tunajivunia na kupata fursa ya kutawala nchi hii.

Nasaha zangu ni kwamba msikae kimya sisi ni vijana wetu mkiona kuna mambo hayaendi sawa tuiteni na kutuelekeza ili tuweze kufanya vizuri zaidi katika utekelezaji wa majukumu yetu.”, alisema Mbeto.

Katibu huyo wa Kamati Maalum ya NEC, Mbeto aliwapongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji mzuri wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020/2025.

Sambamba na hayo Mbeto, alisema kipaumbele chake ni kuhakikisha Chama Cha Mapinduzi Zanzibar kinasema na kutangaza fursa na mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa na Serikali katika kuwatumikia wananchi.

Alieleza kuwa lengo la ziara hiyo ni kuwafariji wazee hao kusherehekea miaka 46 ya kuzaliwa kwa CCM.

Wakizungumza kwa wakati tofauti Wazee hao walishukru uamuzi wa CCM kumruhusu Katibu huyo wa NEC kuwatembelea katika maeneo yao kwa lengo la kuimarisha Umoja na Mshikamano.

Walishauri kuwa viongozi wa Chama wahakikishe wanalinda tunu ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 pamoja na Muungano wa Serikali mbili ili vizazi vijavyo virithi serikali iliyopiga hatua kubwa kimaendeleo.

Wazee hao walieleza kwamba lengo la Afro Shiraz Party ni kuondosha vitendo vyote vya dhuruma,ukatili na umasikini kwa Wananchi wa Zanzibar hivyo misingi hiyo inatakiwa kuendelezwa kwa vitendo na CCM pamoja na Serikali zake.

Mapema Katibu huyo alitembelea Radio ya CCM ya Bahari FM pamoja na kuzungumza na Watumishi wa CCM Wilaya ya Mjini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.