Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman (wakatikati mwenye treki
manjano) akishiriki katika mazoezi ya viungo na wanavikundi vya Mazoezi kutoka
mikoa mbali mbali ya Tanzania Bara na Zanzibar baada ya kumaliza mazoezi ya
kutembea yaliyoanza Muembe Kisonge na Kumalizikia Uwanja wa Amaan mjini
Zanzibar leo tarehe 04. 02.03 .Picha na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa
Zanzibar kupitia Kitengo chake cha Habari.
Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman akizungunza na wanavikundi
vya Mazoezi kutoka mikoa mbali mbali ya Tanzania Bara na Zanzibar baada ya kumaliza mazoezi ya kutembea
yaliyoanza Muembe Kisonge na Kumalizikia Uwanja wa Amaani mjini Zanzibar leo
tarehe 04.02.03. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar).
Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman (mwenye treki manjano) akimkabidhi
cheti cha Ushiriki Ernest Mosses kutoka kikundi cha Far East Joging group &
Sport Club baada ya kushiriki katika mazoezi ya kutembea kuanzia Muembe Kisonge na kumalizikia Uwanja wa Amaan
mjini Zanzibar leo tarehe 04.02.2023.Picha na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais
wa Zanzibar kupitia Kitengo chake cha Habari.
Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman (wakatikati mwenye treki
manjano) akishiriki katika mazoezi ya kutembea pamoja na wanavikundi vya
Mazoezi kutoka mikoa mbali mbali ya Tanzania Bara na Zanzibar yaliyoanzia Muembe Kisonge na Kumalizikia Uwanja wa Amaan
mjini Zanzibar leo tarehe 04.02.2023.Picha na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais
wa Zanzibar kupitia Kitengo chake cha Habari.
MAKAMU wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Othman Masoud Othman, ameitaka jamii kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi ili
kusaidia kujenga afya na kuepusha nchi kutumia gharama kubwa kuwatibu wananchi
kwa maradhi yasiyoambukiza.
Mhe. Othman
ameyasema hayo huko uwanja wa Amaan
mjini Zanzibar alipozungunza katika Bonanzala kutumia miaka 18 tokea
kuanzishwa kwa kikundi cha mazoezi cha Amani mjini Zanzibar baada ya kushiriki
katika Matembezi ya mazoezi kuanzia Muembe Kisoinge na kumalizikia uwanja wa Amaan ambayeo yalivishirikisha
vikundi mbali mbali kutoka Zanzibar na Tanzania bara.
Amefahamisha
kwamba kufanya mazoezi ni uwekezaji mkubwa kwa nchi na jamii katika kutibu na kuweka kinga ya maradhi
mbali mbali yatokanayo na mfumo wa ulaji na lishe isiyona mpangilio sahihi wa
kitaalamu na kuchangia wananchi waliowengi kupata maradhi kama vile kisukari,
sindikizo la damu na mengineyo.
Mhe. Makamu
amesama kwamba serikali kupitia tasasisi
zake mbali mbali inaunga mkono jitihada za wananchi wanaojitokeza katika
kujumuika kwenye mazoezi mbali mbali jambo
ambalo ni muhimu kwa afya zao na kupunguza gharama za matibabu kwa taifa.
Mhe. Othman
amewataka wananchi kuhakikisha kwamba wanajenga utamaduni wa kupima afya zao
kwa angalau mara moja kwa mwaka jambo ambalo litasaidia kujua hali zao na kuwa
na thahadhari juu ya kujikinga na maradhi yatokanayo na vyakula hasa vya mafuta
na sukari katika kiwango kikubwa kuliko inavyohitajika.
Aidha Mhe.
Othman amewataka wananchi hasa wenye umri kubwa kuhakikisha kwamba wanaacha
kula kwa wingi vyakula vya mafuta mengi
ikiwemo unywaji wa supu za makongoro na mengineyo ambayo yanaweza kuleta
madhara kwa afya zao.
Mhe. Makamu
amewapongeza wanavikundi hao na kuwataka kuhakikisha kwamba wanafanya juhudi
kubwa za kujenga uelewa kwa jamii ili wananchi waliowengi waweze kushiriki
katika mazoezi ya aina mbali mbali ili
kulinda afya zao na kujiepusha na maradhi mbali mbali.
Naye
Mwenyekiti wa Klabu ya Mazoezi ya Amaan ndugu Ibarahim Chagua Abdalla, amesema
kwamba Klabu hiyo imepata mafanikio makubwa kwa wanamicho kupunguza unene na
kutoa wito kwa wananchi katika maeneo mbali mbali kujiunga na vikundi tofauti
vya mazoezi ili kuisaidia taifa katika kupambana na maradhi yasiyoambukiza.
Katika
risala yao ya wanamazoezi wa Klabu ya Amaan iliyosomwa ndugu Asmahani Yahya,
amesema kwamba klabu hiyo, mbali na kufanikiwa katika kuendeleza shughuli za
mazoezi, lakini pia imekuwa ikijitolea katika kusaidia shughuli mbali mbali za
kijamii ikiwemo utoaji wa damu kuwasaidia wagonjwa.
Katika mazoezi hayo yaliyoanzia Muembe Kisonge Mjini Unguja vikundi viulivyoshiriki vilitoka Mkoa wa Morogoro, Dodoama, Dar es Salaam na wenyeji Zanzibar viliongozwa na Klabu ya mazoezi kutoka Amani mjini Zanzibar.
Imetolewa
na Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kupitia Kitengo chake cha
Habari leo tarehe 04.02.2023
No comments:
Post a Comment