Habari za Punde

Rais Dk Hussein Mwinyi afungua Maonesho ya Utalii na Uwekezaji Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikata utepe kuyafungua Maonesho ya Utalii na Uwekezaji Zanzibar,yanayofanyika katika viwanja vya jengo la Makumbusho  Mnazi mmoja  Wilaya ya Mjini Unguja   “ Baitul Amaan “ (kushoto kwa Rais) Mke wa Rais Zanzibar Mama Mariam Mwinyi, Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said na (kulia kwa Rais) Mwenyekiti wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Bw. Rahim Bhaloo na Katibu Mtendaji Kamisheni ya Utalii Zanzibar Bi. Hafsa Mbamba.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika ukumbi wa Jengo la Makumbusho Mnazi Mmoja “Baitul Amaan” Wilaya ya Mjini Unguja wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Utalii na Uwekezaji Zanzibar, ukipigwa wimbo wa Taifa, na (kushoto kwa Rais) Mwenyekiti wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Bw. Rahim Bhaloo na Mke wa Rais wa Zanzibar.Mama Mariam Mwinyi na Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrissa Mustafa Kitwana na (kulia kwa Rais) Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe.Simai Mohammed Said, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Mohammed Said Mohammed (Dimwa) (Picha na Ikulu)
WAGENI Waalikwa katika hafla ya ufunguzi wa maonesho ya Utalii na Uwekezaji Zanzibar wakiwa katika ukumbi wa jengo la Makumbusho Mnazi Mmoja “Baitul Amaan” Wilaya ya Mjini Unguja  wakati ukipigwa wimbo wa Taifa kabla ya kuaza kwa hafla ya ufunguzi huo uliofanyika leo 9-2-2023.(Picha na Ikulu)
MSANII wa Kikundi chaTaarab  Rahatul Zamani Bw.Nassor Abdallah (Cholo Ganuni) akitumbuiza wakati wa hafla ya ufunguzi wa Maonesho ya Utalii na Uwekezaji Zanzibar, yanayofanyika katika viwanja vya Makumbusho Mnazi Mmoja  “Baitul Amaan” Wilaya ya Mjini Unguja, yaliyofunguliwa leo 9-2-2023 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi .(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia na kuyafungua Maonesho ya Utalii na Uwekezaji Zanzibar, yanayofanyika katika viwanja vya Makumbusho Mnazi Mmoja “Baitul Amaan” Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar leo 9-2-2023.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi Cheti cha Shukrani Mwakilishi wa Shirika la Ndege la Qatar Airways Bi.Pamela Sookhai, kwa mchango wao wakati wa hafla ya ufunguzi wa Maonesho ya Utalii na Uwekezaji Zanzibar, yanayofanyika katika viwanja vya Makumbusho Mnazi Mmoja "Baitul Amaan" Zanzibar Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
BAADHI ya Mabalozi Wadogo waliopo Zanzibar na Wageni waalikwa wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, akihutubia katika hafla ya ufunguzi wa Maonesho ya Utalii na Uwekezaji Zanzibar,uliyofanyika katika ukumbi wa jengo la Makumbusho  Mnazi Mmoja “Baitul Amaan” Zanzibar,  Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar leo 9-2-2023.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Hope & Joy Fashion Shop-Tradtional Clothes, Toys for Kids.Bi. Joyce Tumaini Mrema wakati wakitembelea maonesho ya Utalii na Uwekezaji Zanzibar, baada ya kuyafungua leo 9-2-2023 katika viwanja vya Makumbusho Mnazi Mmoja “Baitul Amaan” Zanzibar Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)
/RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakimsikiliza Mfanyakazi wa Makumbusho Zanzibar Bi.Zuhura Ali,akitowa maelezo ya ujenzi wa nyumba za zamani na mchezo  wa bao, wakati akitembelea maonesho ya Utalii na Uwekezaji Zanzibar, baada ya kuyafungua leo 9-2-2023 katika viwanja vya Makumbusho Mnazi Mmoja “Baitul Amaan “ Zanzibar Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar.Mhe.Simai Mohammed Said.(Picha na Ikulu)
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.