Habari za Punde

Watendaji wa Dawati la Kijinsia Kufanya Kazi Zao kwa Ushirikiano na Uaminifu - Bi.Siti

Na Maulid Yussuf WMJJWW. Zanzibar 

Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Bi.Siti Abbas Ali amewataka watendaji wa dawati la jinsia kufanya kazi zao kwa mashirikiano na uwaminifu ili kusaidia kupunguza kesi za udhalilishaji nchini.

Bi Siti ameyasema hayo katika mkutano wa pamoja  na watendaji wa dawati la jinsia kwa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, katika ukumbi wa dawati la polisi Madema, ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za kuelekea siku ya mwanamke duniani.

Amesema Wizara ya Maendeleo ya Jamii haiwezi kufanya kazi peke yake na ndio maana ikaweka madawati ya kijinsia pamoja na waratibu na wadau balimbali ili kuona inafikia malengo yake.

Mkurugenzi siti ameawataka watendaji hao wa madawati kuhakikisha wanazimamia vyema kesi zinapofikishwa vituoni mwao kwa kuona zinafika Mahakamani na kutolewa hukumu.

Pia amewataka kuwapa  ushauru mzuri kwa wale wanofika vituoni mwao kwa kutoa malalamiko yao kwani wengi wao wanakuwa na presha na hofu kutokana na matatizo yanapowafika.

Nae Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Mjini Magharibi  Mkaguzi wa Polisi Mohammed Mwadini Kificho, amesema January mwaka huu wa 2023 matukio ya udhalilishaji  yaliyoripotiwa katika vituo vyao yameongezeka ukilinganisha na mwaka jana ambapo January ya mwaka jana kumeripotiwa jumla ya matukio 19 huku January ya mwaka huu ikiwa kumeripotiwa jumla ya matukio 99 katika Mkoa wa mjini Magharibi. 

Amesema hali hiyo imetokana na uhamasishaji wa utoaji wa elimu juu ya kuyaripoti matukio hayo na yanotokea na sio kukaa kimya ingawa hali hiyo inaiathiri jamii.

Kwa upande wao Watendaji wa dawati la jinsia wamesema kuripotiwa kwa matukio ya udhalilishaji katika kipindi cha mawio kunawapa ugumu juu ya kuendeleza kesi kwani mtuhumiwa anakimbia.

Hata hivyo wameiomba jamii kuacha umuhali kwa kuwafichua watendaji wa matukio hayo kutokana na kesi nyingi zinazoripotiwa zinatoka ndani ya familia au watu wa karibu na maeneo yao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.