Habari za Punde

Benki ya NMB Kanda ya Zanzibar Yaadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa Kukabidhi Msaada wa Vyakula kwa Wanawake Wajane

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Zanzibar Bi.Naima Said Shaame akijumuika katika kukata Keki ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyoadhimishwa leo 8-3-2023 na Benki ya NMB Kanda ya Zanzibar, Tawi la Darajani Unguja na (katikati) Mama Mjane Bi. Tatu Haji Khamis na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wajane Zanzibar Bi.Tabia.Makame Mohammed, Maadhimisho hayo yaliofanyika katika Tawi la NMB Darajani Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar. 

Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Zanzibar Bi.Naima Said Shaame,  akimlisha keki Mama Mjane Bi.Tatu Haji Khamis wakati wa sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyoadhimishwa leo 8-3-2023, Benki ya NMB imeadhimisha kwa kutowa Msaada wa Vyakula kwa Wanawake Wajane Bi.Tatu Haji Khamis wa Kijiji cha Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wajane Zanzibar.Bi.Tabia Makame Mohammed. Maadhimisho hayo yaliyofanyika katika Benki ya NMB Darajani Unguja Jijini Zanzibar.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wajane Zanzibar Bi.Tabia Makame Mohammed akiwalisha Keki ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Mama Wajane wakati wa hafla ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake iliyoadhimishwa na Benki ya NMB Kanda ya Zanzibar Tawi la Darajani Unguja Jijini Zanzibar leo 8-3-2023, na kukabidhi msaada wa vyakula kwa Wanawake Wajane wa Kijiji cha Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja.
MENEJA wa Benki ya NMB Kanda ya Zanzibar.Bi. Naima Said Shaame (kulia) akimkabidhi msaada wa Vyakula Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wajane Zanzibar.Bi.Tabia Makame Mohammed, kwa ajili ya Wanawake Wajane wa Kijiji cha Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja, kwa ajili ya Wanawake Wajane wa Kijiji cha Matemwe, Benki ya NMB imeadhimisha Siku ya Wanawake Duniani kwa kutowa msaada wa vyakula kwa Wanawake Wajane.


  
NENEJA wa Benki ya NMB Kanda ya Zanzibar B.Naima Said Shaame akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wajane Zanzibar Bi. Tabia Makame Mohammed (kulia kwake) pamoja na Wafanyakazi wa NMB, wakati wa hafla ya Maadhimusho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyoadhimishwa leo 8-3-2023.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.