Alisema jamii ya wanawake wengi imekubwa
na taharuki ya kukimbizana na harakati za uchumi na kujitafutia maisha huku
jukumu la ulezi likipewa mgongo hali aliyoieleza inaathiri sana watoto kwenye
ustawi wa makuzi yao bila ya uwepo wa mama karibu.
Mama Mariam Mwinyi aliyasema hayo
kwenye ufunguzi wa kongamano la siku ya Wanawake duniani lililofanyika ukumbi
wa Sheikh Idrisa Abdul Wakil, Kikwajini wilaya ya wijini, Mkoa wa Mjini Magharibi.
Alisema mwanamke ana wajibu mkubwa
wa ulezi wa familia na jamii katika mipango yake yote anayojipangia lazima
atenge muda kwa ajili ya watoto wake.
“Katika mipango yote tunayoipanga
lazima tuhakikishe tunalizungumzia suala zima la nafasi ya malezi kwa mwanamke,
tunapokimbizana sana na uchumi katika miaka hii ya karibuni pametokea mwanya wa
malezi kwa watoto, lazima tutenge muda kwaajili ya watoto wetu haijaalishi
nafasi gani mwanamke yupo kwenye karakati zake, uwe Waziri au Mkurugenzi
tuhakikishe watoto tunawapa nguvu na tunawaelekeza. Aliasa mama Mariam Mwinyi.
Alisema wanawake wako kwenye sekta
zote za uchumi, wanafanya kila linalowezekana kwaajili matunzo ya familia zao.
Alisema katika harakati za kukabiliana
na usawa wa kijinsi na kujikwamua kiuchumi kwa hali zote, wanawake wamekuwa
wamebanwa na harakati hizo hivyo aliwaeleza kujua wajibu wao wa ulezi kwa watoto
wao.
“Tusije tukakimbizana sana hili
jambo la malezi tukalisahau sababu mwalimu wa kwanza duniani kwa mtoto ni mama,
ni sisi ndio tunaobaki nao majumbani, mama ndie rafiki bora kwa mtoto, mama ni
daktari wa kwanza nyumbani, duniani kwa mtoto ni mama, mama ndie anaetoa huruma
kwa watoto wake, mtoto akiumia pale unapomwambia pole mwanangu, anapata hisia
mama ndio kila kitu kwake, lazima tujichanganye kwenye muda wa kutafuta wakati
huo huo ulezi wa familia.” Alisisitiza Mama.
Alisema kauli mbiu ya siku ya
wanawake duniani mwaka 2023 inachanganua na kuwasisitiza wanawake wawe
wadadisi, wajasiri, wajasiriamali na wabunifu na wenye kuleta mabadiliko yatakayo
kabiliana na umasikini, haki, ukosefu wa kipato kwa jamii na taifa kwa ujumla
kwa kutumia njia sahihi za teknolojia.
Aidha, Mama Mariam Mwinyi aliwashauri
wanawake na kinamama kujitahidi kutumia fursa zinazopatikana kupitia teknolojia
ya kisasa kwa kijitangaza kibiashara na kutumia soko la kimtandao kwajili ya
kutangaza bidhaa na kazi za vikundi vyao ili kupata maendeleo ya haraka.
Pia, aliwashauri wazazi na walezi
majumbani kuwashauri na kuwanasihi watoto wapende sana masomo ya sayansi ili
kuwajenga mapema kuwa watoto wazuri wa teknolojia ya baadae, kwa kuwaungamkono
na kuwasaidia kwenye masomo ya sayansi na hesabati badala ya kuwaachia na kuwa
watoto wakawaida.
Alisema wazazi/walezi wanapaswa
kutumia kigezo cha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu
Hassan kuwa kigezo bora kuzifikia ndoto za watoto wao kwa kuwapa moyo ili
nabidii kwenye masomo yao ili waje wafuate nyayo za Rais Samia.
Alisema Serikali ya mapinduzi ya
Zanzibar inaunga mkono matumizi ya teknolejia kwa kuweka miundombinu bora ya
teknolojia kwenye madarasa ya shule za msingi ili kuwajenga mapema watoto
kiteknolojia.
Akizungumzia umuhimu wa bima, Mama
Mariam Mwinyi aliitaka jamii kuona umuhimu wa kukata bima kwaajili ya kujikinga
na majanga. Aidha, aliwataka Mamala ya Usimamizi wa Bima Tanzania TIRA kuongeza
bidii ya kutoa miongozo na elimu kwa umma juu ya umuhimu wa kuwa na BIMA nchini.
Akizungumza kwenye hafla hiyo kwa
niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Uchumi, Dk. Sada Mkuya Salum,
Naibu wa Wizara hiyo, Ali Suleiman Mrembo alisema Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar na ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania zinadhamira njema kuhakikisha
usawa wa kijinsia unakwenda sambamba kwenye kuleta maendeleo ya Watanania wote.
Alieleza Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar, imeelekeza mipango na sheria, miongozo na taratibu zake kuona usawa
wa jinsia kwenye teknolojia unakuwa chachu ya ukombozi wa wanawake.
Naye, Naibu Waziri wa Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wanawake na Watoto, Ana Anatasi Paul, aliwashauri wanawake
kupitia vikundi vya wajasiriamali na kinama kuitumia teknolojia kwa kujitangaza
na kujitoa kiuchumi. Alisema wanawake walio wengi bado wako nyuma na matumizi
ya tenkolojia, aliwashauri kuitumia fursa hiyo kujikwamua kiuchumi na kutangaza
biashara zao na kulitumia vyema soko la teknolojia.
Kwa upande wake, Naibu Kamishna wa
Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Khadija Issa alisema mafanikio ya
shirika hilo yalichangiwa na ubunifu wa elimu jumuishi pamoja na njia za kisasa
za usambazaji wa bima aidha, alieleza malengo ya Mamlaka hiyo kwa kushirikiana
na wadau wake ikiwemo kutoa elimu kwa umma, kunzisha na kutekeleza mpango wa bima
ya kilimo, uimarishaji na uunganishaji wa mifumo ya taasisi mbalimbali za
serikali zikiwemo jeshi la polisi mamlaka za bandari, mamlaka zote za mapato
nchini.
Pia, aliiomba Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar kuipa ushirikiano mamlaka hiyo kwenye kutekeleza malengo yake hayo.
Kongamano hilo la siku ya wanawake
duniani lilitayarishwa na Mamkala ya Usimamizi wa Bima, Tanzania, TIRA.
No comments:
Post a Comment