Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza na
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, David Concar, Ikulu Zanzibar.
Dk. Mwinyi, alieleza
Serikali imedhamiria kuifungua Pemba zaidi kwa maendeleo makubwa mara tu
baada ya kukamilika kwa ujenzi mpya wa uwanja wa ndege wa kimataifa ili kuweka uwiano sawa na
mandhari ya kisiwa cha Unguja kwa uondoa utofauti wa maendeleo uliopo baina yao.
“Ki maendeleo Unguja na Pemba
hazipo sawa, tunataka kuibadilisha Pemba kuwa sawa na Unguja kimaendelo”
aliahidi Dk. Mwinyi.
Alisema ujenzi wa barabara
kutoka Chake hadi Mkoani na Ujenzi wa uwanja wa ndege mpya kwa sasa ni miradi
mikubwa ya maendeleo kisiwani humo ambayo ni muhimu sana kwa Zanzibar.
Dk. Mwinyi alisema tayari Serikali
imefikia hatua nzuri ya mazungumzo baina yao wakandarasi wa ujenzi huo na
kueleza tayari mchakato wa awali wa ujenzi wa jengo la taminali kwa uwanja wa
ndege umeanza.
Alisema kukamikika kwa miradi
hiyo kutaifungua zaidi Pemba kimaendeleo kwa kuruhusu ndege kubwa za kimataifa
kutua kisiwani humo.
Naye Balozi Concer alieleza
dhamira ya Uingereza kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika ushirikiano
wao wa miradi hiyo ya Pemba, alisema mchakato wa fedha upo tayari kutoka kwa hazina
kuu ya Uingereza na kusisitiza matarajio yake ya kuanza haraka kwa ujenzi huo.
Aidha, Balozi Concer alimuahidi Rais
Mwinyi kwamba Serikali ya Uingereza na Zanzibar wataendeleza ushirikiano uliopo
katika kukuza Sekta za maendeleo na kuimarisha uhusiano wao kidipolomaisia
uliopo baina yao.
Uhusiano wa diplomasia baina
ya Tanzania na Uingereza ni wa kihistoria, ambao umeimarika zaidi kwenye sekta za
biashara, kilimo, madini na viwanda na kutajwa kuwa Uingereza ni mwekezaji mkubwa
wa kigeni kwenye sekta hizo.
Tanzania
ikiwa mwanachama wa Jumuiya ya Madola (Commonwealth) pia ni mshirika mzuri na
Uingereza tokea mwaka 1964, kwasasa ina balozi wake Dar es Salaam,
David Concar tangu mwaka 2020 na Tanzania balozi wake nchini Uingereza ni Dk. Asha
Rose Migiro. Mataifa
mawili yameendelea kuimarisha uhusiano baina yao kwa fursa nyingi za maendeleo
kupatikana pande mbili hizo ikiwemo Zanzibar.
IDARA YA MAWASILINO, IKULU ZANZIBAR
Safi Sana zanzinews kwa habari na taarifa zakutosha.
ReplyDelete