Habari za Punde

Kliniki za Sikoseli Kuazishwa Katika Hospitali za Wilaya Zanzibar

Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui akizungumza na madaktari pamoja na wazazi wa watoto wenye ugonjwa wa mifupa (SICKEL SELL) katika maadhimisho ya siku ya sikoseli Duniani ambayo haudhimishwa kila ifikapo juni 19,hafla iliyofanyika Skuli ya Maandalizi Kidutani

Na fauzia Mussa  Maelezo

Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui amesema Wizara inakusudia kuweka  kliniki maalum za wagonjwa wa mifupa (SICKEL CELL)  katika hospitali za Wilaya ili kupunguza changamoto ya kufuata huduma hizo  katika hospitali ya Mnazimmoja.

Ameyasema hayo wakati akipokua akizungumza na madaktari pamoja na  wazazi wa watato wenye ugonjwa huo  katika maadhimisho ya  siku ya sikoseli yaliofanyika Skuli ya maandalizi Kidutani Mjini Unguja.

Alisema kwa sasa zanzibar ina wagonjwa zaidi ya mia mbili wanaojulikana  wa sikoseli hivyo hatua ya kuanzishwa kliniki katika hospitali za Wilaya kutawapunguzia mzigo  Hospitali ya Mnazimmoja na kuwaacha wakihudumia wagonjwa walioshindikana katika hospitali za Wilaya na Mkoa.

Akizungumizia suala la upatikanaji wa damu salama ambayo ndio hitajio kubwa la wagonjwa hao Waziri mazrui alisema upatikanaji wa damu bado ni mdogo kulingana na mahitaji hivyo ameitaka jamii kujitokeza na kushajihishana kuchangia damu ili kuokoa maisha ya watu hasa watoto wanaoishi na ugonjwa wa mifupa kwani wao ndio wahitaji wakubwa.

"Ipo haja sasa ya kuchangishana damu kama tunavyochangishana katika mambo mengine ili tuokoe maisha ya wagonjwa wa sikoseli na kujiwekea akiba sisi wenyewe kwani pia niwahitaji watarajiwa." Alisisitiza Waziri Mazrui

Mapema Waziri mazurui aliutaka Uongozi wa Hospitali ya Mnazimmoja kuhakikisha  maadhimio waliojiwekea yanatimia ikiwemo kujenga na kuimarisha jumuiya za kilimwengu za seli mundu pamoja na kurasimisha uchunguzi wa watoto wachanga wanapozaliwa ili kujua Hali ya ugonjwa wa sikoseli.

Alifahamisha kuwa maadhimisho hayo yanafanyika si kwaajili ya kufurahia uwepo wa ugonjwa huo Bali ni kwa ajili ya kujuana , kuweka na kusimamia mikakati ya kukabiliana na ugonjwa huo.

Katika kuhakikisha watoto hao wanatambulika na kupata misaada mbalimbali Waziri Mazrui  aliwataka Madaktari  kwa kushirikiana na wazazi wa watoto hao kuanzisha jumuiya maalum ili kuweza kutambulika na kupata misaada mbalimbali kutoka kwa wafadhili wa nje na ndani  ya nchi.

"Kipimo kimoja cha kupima selimundu kwa mtoto mchanga kinagharimu   elfu13 , tukiwa na jumuiya  kutapelekea kupata Misaada angalau wa hivi vipimo vya kuchunguzia ugonjwa huu kwa  watoto wetu mara tu wanaozaliwa  kama tunavyowachunguza  virusi vya ukimwi" alishauri waziri mazurui.

Vile vile aliwataka wanandoa watarajiwa kuchunguza afya zao kwa kuangalia hali ya sikoseli kabla ya ndoa kwani  endapo wazazi watakua na ugonjwa huo Wana nafasi kubwa ya kurithisha kizazi kitakachozaliwa .

"Tuache kuendekeza mapenzi ifike wakati tuchunguzane sikoseli kama tunavyochunguzana ukimwi kabla ya ndoa,hii itasaidia  kupungua kwa watoto wanaorithishwa sikoseli kutoka kwa wazazi wao" alisisitiza Mazurui
sambamba na hayo Waziri Mazrui aliwashukuru madaktari kwa kuwapatia huduma bora watoto  hao pamoja na wazazi wanaoendelea kuwatunza kwani kuna baadhi ya wazee huwatelekeza mara baada ya kugundua ni wagonjwa.

Nao wazazi wa watoto wanaoishi na ugonjwa huo Wameiomba Wizara kutowakuwachanganya  watoto wao katika wodi ya watu  wazima wafikapo umri wa miaka 13 kwani bado ni wadogo na wanahitaji kuwa karibu na wazazi.

Aidha waliushauri Uongozi wa Hospitali ya Mnazimmoja  kuweka wodi maalum kwaajili ya watoto wenye ugonjwa huo wenye umri wa kuanzia miaka 13 Hadi 18 ili waweze kuwa nao karibu katika kipindi kigumu cha ugonjwa.

Dunia huadhimisha siku  ya Ugonjwa wa SICKEL CELL kila ifikapo Juni 19 kwa lengo la kuwajengea uelewa na kufanya ukaguzi wa afya kwa watu mbali mbali ili kuchukua tahadhari za mapema juu ya ugonjwa huo,
Kauli mbiu "VUNJA MDUARA,PIMA JUWA HALI YAKO YA SIKOSELI"
Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui akizungumza na madaktari pamoja na wazazi wa watoto wenye ugonjwa wa mifupa (SICKEL SELL) katika maadhimisho ya siku ya sikoseli Duniani ambayo haudhimishwa kila ifikapo juni 19,hafla iliyofanyika Skuli ya Maandalizi Kidutani
Mkurugenzi Tiba Hospitali ya Mnazimmoja Dkt.Marijani Msafiri akizungumza machache na kumkaribisha mgeni Rasmi Waziri wa Afya Nassor Ahmed Mazrui kuzungumza na wazazi wa watoto wenye ugonjwa wa mifupa (SICKEL CELL) wakati wakiadhimisha siku ya ugonjwa huo ambao huadhimishwa kila ifikapo juni 19 Duniani kote ,hafla iliyofanyia Skuli ya Maandalizi Kidutani.
Shujaa  Hajji Ally Issa akitoa elimu fupi kuhusiana na  ugonjwa wa sikoseli (SCD) wakati wa maadhimisho ya  siku ya ugonjwa huo ambayo huadhimishwa kila ifikapo Juni 19 Duniani kote ,hafla iliyofanyika Skuli ya Maandalizi Kidutani

Wananchi mbalimbali wakipata huduma za kuangalia afya katika maadhimisho ya siku ya sikoseli ambayo huadhimishwa kila ifika juni 19 Duniani kote Huko Skuli ya Maandalizi Kidutani Mjini Unguja.
Wananchi mbalimbali wakipata huduma za kuangalia afya katika maadhimisho ya siku ya sikoseli ambayo huadhimishwa kila ifika juni 19 Duniani kote Huko Skuli ya Maandalizi Kidutani Mjini Unguja
Wananchi mbalimbali wakipata huduma za kuangalia afya katika maadhimisho ya siku ya sikoseli ambayo huadhimishwa kila ifika juni 19 Duniani kote Huko Skuli ya Maandalizi Kidutani Mjini Unguja.
Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui  akiwa katika picha ya pamoja na watoto wenye ugonjwa wa sikoseli katika maadhimisho ya siku ya ugonjwa huo amabayo huadhimishwa kila ifikapo juni 19.hafla iliyofanyika Skuli ya Maandalizi Kidutani.
PICHA NA FAUZIA MUSSA-MAELEZO ZANZIBAR.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.