Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Mwinyi Azungumza na Ujumbe wa UNESCO Ikulu Zanzibar

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Mkurugenzi Mkaazi wa UNESCO Kanda ya Afrika Mashariki.Prof Hubert Gijzen, alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo yaliyofanyika leo 15-6-2023 katika ukumbi wa Ikulu akiwa na Ujumbe wake.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na mgeni wake Mkurugenzi Mkaazi wa UNESCO Kanda ya Afrika Mashariki Prof. Hubert Gijzen (kulia kwa Rais) akiwa na Ujumbe wake walipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu leo 15-6-2023.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itatoa ushirikiano wa hali ya juu kwa Shirika la kimataifa la UNESCO kwenye masuala yote inayoyasimamia ikiwemo hifadhi ya kimataifa ya Mji mkongwe, sekta za Afya na Elimu.

Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa ushirikiano na Serikali ya Oman wanaendelea kusimamia ujenzi wa jengo la “Bait el Ajaab” pamoja na nyumba ya “People Palace”

Dk. Mwinyi aliyasema hayo alipozungumza na ugeni kutoka shirika la kimataifa la UNESCO, uliofika Ikulu, Zanzibar kwa mazungumzo.

Rais Dk. Mwinyi aliishukuru UNESCO kwa kuahidi kuongeza nguvu kwenye ujenzi wa majengo hayo na kuwaondolea hofu ya kubadilishwa uhalisia wa majengo hayo baada ya marekebisho.

Dk. Mwinyi aliueleza uongozi wa UNESCO kwamba licha ya maboresho makubwa yanayofanywa kwenye ujenzi wa majengo hayo, Serikali inasimamia kwa karibu na kuhakikisha thamani na mali zote za asili zilizokuwemo kwenye majengo hayo zinarushishwa sehemu husika.

Pia Dk. Mwinyi aliieleza UNESCO dhamira ya Serikali kuwajengea uwezo wa kujikimu na kujiendeleza kimaisha vijana wa Zanzibar watakaomaliza masomo yao, kwa kupewa elimu ya ujasiriamali na ubunifu tokea wakiwa masomoni.

Alieleza nia ya Serikali kubadili mfumo mzima wa elimu ya Zanzibar ili uwe wezeshi kwa wanafunzi wanaomaliza masomo wanaporudi kwenye jamii zao wawe na uwezo wa kujikimu kimaisha.

Mwakilishi mkaazi wa UNESCO kutoka kanda ya Afrika Mashariki, Prof. Hubert Gijzen aliihakikishia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwamba UNESCO inaungamkono ushirikiano wa Oman na Zanzibar kwenye matenegnezo ya majengo hayo nakuahidi kushiriki kikamilifu kwenye ujenzi huo.

Alisema, licha ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Oman kutoa nguvu kubwa ya ujenzi huo, UNESCO pia inawajibu mkubwa wa kushirikiana na serikali mbili hizo.

Prof. Hubert alitumia fursa hiyo kumueleza Rais Dk. Mwinyi dhamira ya UNESCO kuandaa mkutano mkubwa wa kimataifa Zanzibar utakaozikutanisha pamoja nchi 32 kutoka mataifa mbalimbali duniani kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yanayohusu afya, elimu na ustawi wa maendeleo ya vijana ikiwemo kuwafunza namna ya kujiajiri watakapomaliza masomo yao ili waondokane na utegemezi kupitia program mbalimbali za maendeleo na ujasiriamali ili kutoa uelewa mpana kwa vijana kujitambua.

Pia, alimweleza Dk. Mwinyi mkutano huo utajadili mustakbali wa mageuzi ya sekta za elimu na afya kwa Zanzibar kwa ngazi za skuli hadi vyuo vikuu na namna ya kuleta mabadiko kutokana na changamoto zilizomo kwenye sekta hizo, hivyo Prof. aliiomba ushirikiano wa Serikali kupitia wizara zake katika kufanikisha mkutano huo.

Katika mazungumzo yake Prof. Hubert aliigusia sekta ya maji na kueleza UNESCO imekusudia kuangalia athari za mabadiliko ya hali ya hewa ili kubaini vyanzo vya maji safi vinavyoathiriwa na mabadiliko hayo.

IDARA YA MAWASILIANO – IKULU, ZANZIBAR.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Mkurugenzi Mkaazi wa UNESCO Kanda ya Afrika Mashariki Prof, Hubert Gijzen, alipofika Ikulu Jijini Zanzibar na Ujumbe wake, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 15-6-2023
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Mkurugenzi Mkaazi wa UNESCO Kanda ya Afrika Mashariki Prof, Hubert Gijzen, alipofika Ikulu Jijini Zanzibar na Ujumbe wake, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 15-6-2023
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhia Majarida ya UNESCO, na Mkurugenzi Mkaazi wa UNESCO Kanda ya Afrika Mashariki Prof. Hubert Gijzen, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 15-6-2023
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akipata maelezo ya Majarida ya UNESCO, kutoka kwa Mkurugenzi Mkaazi wa UNESCO Kanda ya Afrika Mashariki Prof. Hubert Gijzen, baada ya kumkabidhi wakati wa mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 15-6-2023, na (kulia kwake) Mkurugenzi Mkaazi wa UNESCO Kusini Mwa Afrika Bi.Lidia.Arthur Brito na Mwakilishi Mkaazi wa UNESCO Nchini Tanzania Ndg.Michel Toto.


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na mgeni wake Mkurugenzi Mkaazi wa UNESCO Kanda ya Afrika Mashariki Prof. Hubert Gijzen, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 15-6-2023.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.