SERIKALI ya Mapinduzi
ya Zanzibar imesema inajivunia ushirikiano wake na Wadau wa Maendelo likiwemo
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Elimu na Watoto
diniani, (UNICEF).
Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi alisema hayo Ikulu,
Zanzibar alipozungumza na Mwakilishi Mkazi wa UNICEF, Tanzania Bi. Shalini
Bahuguna aliefika kwaajili ya kumuaga baada ya kumaliza kwa muda wake wa
utumishi kwenye shirika hilo.
Dk. Mwinyi alisema, Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar inaridhishwa na kazi kubwa inayofanywa na timu nzima
ya UNICEF, Tanzania kupitia ushirikiano wake kwani wako bega kwa bega katika
kuimarisha masuala yanayohusu ustawi wa watoto nchini.
“UNICEF imefanya
makubwa Tanzania hususani ushirikiano wake wa karibu katika kuiungamkono
Serikali yetu kwenye masuala mbalimbali ya maendeleo, wamefanya mengi siwezi
kuyaonesha maeneo yote sababu ni mengi mno.” alifafanua Rais Dk. Mwinyi.
Pia Dk. Mwinyi,
alimpongeza Bi. Shalini kwa jitihada zake, kwa kipindi chote alichofanyakazi na
UNICEF hapa nchini akieleza mchango mkubwa walioutoa kwa Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar hasa katika miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na shirika hilo
katika kuiunga mkono SMZ.
Dk. Mwinyi alimweleza
Mwakilishi huyo kwamba, daima Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kulishukuru
Shirika la UNICEF kwa kuiunga mkono Zanzibar kwenye masuala ya Afya na Elimu.
Akizungumza kwenye
hafla hiyo, Bi. Shalini alimpongeza Rais Dk. Mwinyi kwa uongozi wake hasa
katika kuzisimamia vema rasilimali za Zanzibar kwenye ujenzi wa maendeleo ya
Wazanzibari wa maeneo yote ya Unguja na Pemba.
Alimsifu Dk. Mwinyi
kuwa Kiongozi wa mfano hasa kwa kukinawirisha kimaendeleo Kisiwa cha Pemba na
mageuzi makubwa aliyofanya kwenye sekta za afya na Elimu Zanzibar.
Vilevile bi Bi.
Shalini ameisifu za Zanzibar kwa kufanikiwa kutekeleza malengo ya Mileniam
kwani imefanikiwa kwenye suala zima la kudumisha usafiwa mazingira kwa maeneo
mengi ya miji.
Akizungumzia
mafanikio katika ustawi wa masuala ya watoto, Mwakilishi huyo wa UNICEF
aliipongeza Serikali ya Dk. Mwinyi na kueleza kuwa Zanzibar imefanikiwa kwa
asilimia 75 kuwarejesha skuli watoto wengi walioacha masomo kwa mazingira
tofauti waliyokumbana nayo kwenye makuzi yao.
UNICEF ni Shirika la
Umoja wa Mataifa (UN) lililoanzishwa tangu mwaka 1946 New York, Marekani, linashughulika
na masuala ya Elimu na Watoto duniani, linafanyakazi kwenye maeneo zaidi ya 190
duniani kote, katika kuwafikia watoto na vijana walio kwenye matatizo kutokana
na majanga mbalimbali kwa kuboresha chanjo kwa watoto na kutoa lishe bora
katika kuimarisha huduma za dharura mbali na mambo mengine yanayowahusu watoto.
IDARA YA MAWASILINO, IKULU ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment