Habari za Punde

Uhusiano na Ushirikiano wa Kihistoria Uliodumu kwa Karne Nyingi Kati wa Wananchi wa Zanzibar na Watu wa India

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Balozi wa India Nchini Tanzania Mhe.Biyana.S.Pradhan, alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika mazungumzo na mgeni wake Balozi wa India Nchini Tanzania Mhe. Biyana.S.Pradhan, alipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi leo amekutana na Balozi wa India nchini Mhe.Biyana S.Pradhan ambapo walizungumzia masuala mbalimbali ya Uhusiano na Ushirikiano kati ya Zanzibar na India.

Katika mazungumzo hayo Dk. Mwinyi alisifu uhusiano na ushirikiano wa kihistoria uliodumu karne nyingi kati wa wananchi wa Zanzibar na watu wa India na kueleza kuwa nchi hizo zina kila sababu ya kuimarisha ushirikiano huo.

“wananchi wa Zanzibar na India tumekuwa katika ushirikiano kwa karne nyingi yafaa kuendelea kubadilishana uzoefu wetu katika hatua za maendeleo tulizofikia” Alisema Dk. Mwinyi.

Kwa hiyo alimueleza Balozi Pradhan kuwa Zanzibar ingependa kuona ushirikiano zaidi katika maeneo ya elimu,afya,miundombinu na Teknolojia ya habari na Mawasiliano ambayo pande hizo zimekuwa zikishirikiana kwa muda mrefu lakini pia kupanua maeneo mapya ya ushirikiano ikiwemo Uchumi wa Buluu.

Aliyataja maeneo kuwa ni pamoja na uwekezaji katika sekta zote ikiwemo ya afya pamoja na sekta ya utalii ambapo Zanzibar ingependa kuona watalii wengi zaidi kutoka nchi za Asia wakiwemo toka India wanatembelea Zanzibar na Tanzania kwa jumla.

Aidha Rais Dk.Mwinyi amemuelezea Balozi huyo kuridhishwa kwake na miradi inayosimamiwa na wataalamu wa kampuni kutoka India jinsi inavyoendelea vyema ukiwemo mradi mkubwa wa Usambazaji wa huduma ya Maji safi na salama katika maeneo kadhaa ya Zanzibar.

Vile vile Rais Dk.Mwinyi amemueleza Balozi huyo kuwa ameipokea kwa moyo mkunjufu taarifa ya Ujio wa Waziri wa mambo ya nchi za nje wa India muda ukapowadia na anamkaribisha sana Zanzibar.

Kwa upande wake Balozi Biyana S.Pradhan alimueleza Rais Dk.Hussein Ali Mwinyi kuwa kupanua maeneo mapya ya ushirikiano ni muhimu katika kuimarisha ushirikiano kati ya India na Zanzibar.

Aliahidi kuyashauri makampuni ya biashara ya utalii nchini mwake kuingiza Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.