Habari za Punde

CAF wakagua miundombinu inayotarajiwa kutumika AFCON 2027 Zanzibar


Na Eleuteri Mangi, WUSM, Zanzibar

Timu ya Wakaguzi ya utayari wa nchi za Kenya Uganda na Tanzania kuhusu utayari wao wa kuwa wenyeji AFCON 2027, leo hii Julai 31, 2023 wapo Zanzibar ambapo wamekagua Uwanja wa Amaan, hospitali ya Mnazi Moja, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume pamoja na viwanja vingine vya mazoezi.

Timu hiyo kutoka Shirikisho la Mpira Afrika (CAF) imezungukia maeneo hayo ikiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania Bw. Wallace Karia na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar Bw Suleiman Mahamud Jabir.

Maafisa wengine kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwemo Kaimu Mkurugenzi wa Michezo Bw. Ally Mayayi na Katibu Mtendaji Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bi. Neema Msitha na kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ni Kamishna Idara ya Michezo Bw, Ameir Mohammed, Katibu Mtendaji Baraza la Michezo Zanzibar Saidi Marine pamoja na maafisa wengine kutoka TFF na ZFF.


 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.