Habari za Punde

Dkt. Saada Mkuya azindua matawi ya PBZ Airport na Tunguu

Waziri wa Nchi - Afisi ya Rais- Fedha na Mipango Hajjat Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum akivuta kitambaa baada ya kulifungua rasmi tawi la PBZ liliopo huko Tunguu Zanzibar
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Watu wa Zanzibar PBZ, Dkt. Muhsin S. Masoud akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Nchi - Afisi ya Rais- Fedha na Mipango Hajjat Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum kwenye ufunguzi wa matawi ya PBZ

Waziri wa Nchi - Afisi ya Rais- Fedha na Mipango Hajjat Mhe. Dkt. Saada Mkuya Salum leo tarehe 07/08/2023 amezindua tawi la PBZ liliopo Airport na Tunguu.
Hajjat Dkt. Saada amesema amefurahishwa na hatua zinazochukuliwa na PBZ za kuwasogezea karibu huduma za kifedha wananchi.
Hajjat Dkt. Saada amesema kituo cha Airport ni kituo pekee ambacho kinatoa huduma zote za kibenki kwa masaa 24 na siku zote za wiki.
Hajjat Dkt. Saada amefurahishwa kwakua PBZ inafanya mabadiliko makubwa ya kimaendeleo.
Aidha Hajjat Dkt. Saada amesema kuwa PBZ inafanya vizuri sana na inaelekea kufikia maono ya Mhe. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt Hussein Ali Mwinyi ni kuona maendeleo yapatikana Nchi ikiwemo kuwasogezea karibu huduma za kifedha na kupatikana kwa urahisi Nchini.
Hajjat. Dkt. Saada amesema kuongezeka kwa watumiaji wa huduma za kifedha hii inatokana na dira ya Maendeleo ya 2050, ilani ya CCM ,Sera ya fedha pamoja na Sera ya Uwekezaji Nchini.
Nae Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Muhsin S. Masoud amesema PBZ inalengo la kuwasogezea wananchi huduma bora za kibenki pia inatoa gawio kwa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na matarajio yao kufungua matawi ndani ya Zanziba, Tanzania na Afrika kwa ujumla. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.