Baadhi ya wanafunzi wa Skuli ya Kijini Sekondari, Matemwe Wilaya ya Kaskazini “A” Mkoa wa Kaskazini, Unguja wlipokuwa wakimsikiliza Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mama Mariam Mwinyi
Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mama Mariam Mwinyi akitoa hotuba huko Skuli ya Kijini Sekondari, Matemwe Wilaya ya Kaskazini “A” Mkoa wa Kaskazini, Unguja kwenye hafla ya kuwagaia wanafunzi wa kike taulo za hedhi Salama.
Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mama Mariam Mwinyi akigawa taulo za kike za hedhi salama kwa wanafunzi
Msarifu
na
Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), Mke
wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mama Mariam Mwinyi
amewahimiza wanafunzi wa Skuli za Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Unguja kuongeza bidii
na maarifa kwenye masomo yao ili kutoa ufaulu mzuri kwa ustawi wa maendeleo ya
maisha yao ya baadae.
Mama
Mariam Mwinyi aliyasema hayo Skuli ya Kijini Sekondari, Matemwe Wilaya ya
Kaskazini “A” Mkoa wa Kaskazini, Unguja kwenye hafla ya kuwagaia wanafunzi wa
kike taulo za hedhi Salama.
Alisema,
hakuna linaloshindikana endapo wataongeza bidii ya masomo yao ili waepukane na
unyanyasaji kwenye jamii zao.
Mama
Mariam Mwinyi alieleza mradi wa ‘Tumaini initiative’ wa ZMBF unaotoa taulo za hedhi
salama, umelenga kufufua ndoto wa wasichana na wanafunzi wa kike kuendelea
kuhudhuria masomo yao kila mwezi bila kukatisha masomo yao hasa wanapokua
kwenye ada zao za kila mwezi.
Aidha,
alieleza taulo hizo zitawapunguzia mzigo wa gharama za matumzi ya kila mwezi
wazazi nawalezi wa wanafunzi hao kwa kipindi cha miaka mitatu hadi mitano
endapo zitatunzwa vizuri pamoja na kuwaweka sakama na afya njema kwani hazina
kemikali.
Alisema
mbali na kutunza afya za wasichana na wanafunzi hao lakini pia kutunza
mazingira kwa kukwepa kutupa taulo ovyo badala zake wazifue na kuzitunza
vizuri.
Hivyo,
aliomba wafadhali zaidi kujitokeza kuufadhili mradi wa ‘Tumaini initiative’ ili
kuwaondoshea mzigo mzito wa uchumi wananfunzi na wazazi kuepuka gharama kubwa
ya kutumia taula za kutupa.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation, Fatma Fungo
alisema lengo la taasisi hiyo ni kuwafikia zaidi ya wanafunzi 20,000 ndani ya
muda mfupi kwa kuwapa taulo za hedhi salama ambapo kwa kipindi cha miezi minne
tayari wamewafikia wanafunzi 1557 wa skuli mbalimbali za Unguja Pemba.
Akizungumza
kwenye hafla hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Ayoub Mahmoud,
Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini ‘A’ Unguja, Sadifa Juma Khamis alieleza masikitiko
yake ya matokeo mabaya ya Skuli ya Kijini Sekondari, Matemwe, hivyo aliitoa
wito kwa walimu na wanafunzi wa Skuli hiyo kuongeza jitihada ili kuibadilisha
hali iliyoposasa kwa kuleta mabadiliko makubwa na matokeo ya mitihani yao ya
Taifa.
Naye,
Mkurugenzi Secondari, Bi Asya Iddi Issa aliwahimiza wanafunzi hao usafi wa afya
zao na mazingira wanayosomea hasa kwenye matumizi ya taulo hizo ili kupata muda
mzuri wa kujisomea.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Taasisi ya Wajamama, inayojishughulisha na kutoa taaluma ya afya ya uzazi,
Dk. Mwanakheir Mahmoud alisema 48% ya wasichana na wanafunzi wa kike hushindwa
kuhudhuria masomo yao ipasavyo Kila mwenzi kutokana na kutokua na hedhi Salama,
aidha alieleza asilimia 28 ya wasichana hawana maarifa ya kujitunza na kutumia
hedhi salama.
Alisema
mbali na kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa jamii lakini pia wamekusudia
kuwafikia zaidi ya wasichana 500 kuwapa elimu ya hedhi salama.
Taasisi
ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) iliasisiwa Julai mwaka 2022 na
kuzinduliwa rasmi Febuari mwaka jana, mwezi Machi mwaka huu, ilizindua Mpango Mkakati
wa miaka mitatu pamoja na mradi wa “Tumaini kit” ambao hadi sasa umefanikiwa
kuzalisha taulo za kike zaidi ya 5000 na kuzisambaza zaidi ya 1500 kwa
wanafunzi na wasichana wa skuli za msingi na sekondari kwa Unguja na Pemba.
Aidha,
taasisi hiyo inafanya kazi kwa karibu na tasisi za Serikali zikiwemo Mahakama
ya Zanzibar, Wizara ya Afya, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Wizara ya
Uchumi wa Buluu, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee Wazee na watoto, Wizara
ya Habari na Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda.
IDARA YA MAWASILIANO IKULU,
ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment