Habari za Punde

Kampuni ya Belgium yataka kuwekeza mitambo ya kuhifadhi samakiWizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi waliupokea ujumbe wa watu watatu kutoka Kampuni ya TSE Belgium ambao wamefika Zanzibar kuangalia fursa za kuwekeza katika mitambo ya kuhifadhi samaki (Cold Storage Facilities) hapa Zanzibar pamoja na fursa nyengine za uwezeshaji katika Uvuvi.

Ujumbe huo ukiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya TSE Belgium Africa Group, Laurent Gueubel, Bwana Marc Huberty ambaye ni Business Developer kutoka Kampuni ya HM, na Patrick Muwowo ambaye ni Regional Strategic Advisor, TSE Africa Group, walifanya mazungumzo na Katibu Mkuu Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Dr. Aboud Suleiman Jumbe pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo na Uratibu wa Uchumi wa Buluu, Ndg Zahor Elkharousy na maafisa watendaji wengine wa Wizara walioshiriki katika Kikao hicho

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.