Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imo mbioni kukimaliza Kiwanda cha kuchakatia mwani kilichopo Chamanangwe Mkoa wa Kaskazini Pemba ambacho kitakuwa ni sulihisho la kilio cha Wakulima wa Mwani Kisiwani Pemba na Zanzibar kwa ujumla.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Ndugu Hemed Suleiman Abdulla ameyasema hayo akizungumza wanachama wa CCM na Wananchi wa Jimbo la Pandani na Jimbo la Kojani akiwa katika muendelezo wa ziara yake ya kuimarisha Chama Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Amesema katika kutekeleza Ilani ya CCM Serikali ipo katika hatua za mwisho kukamilisha ujenzi wa Kiwanda cha kusarifia Mwani kilichopo Chamanangwe Mkoa wa Kaskazini Pemba ambacho kitawanufaisha Wakulima wa Mwani na kitatoa fursa nyingi za ajira kwa wananchi.
Amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itahakikisha zao la mwani linauzwa kwa bei ya juu hapa hapa Nchini hivyo amewataka Wananchi wa kisiwani Pemba waitumie vyema fursa hiyo ili kujikwamua na ukali wa maisha.
Aidha ameeleza kuwa wakulima wa zao la mwani Serikali kupitia mfuko wa uwezeshaji wananchi kiuchumi itawawezeshwa vifaa vyote vya kulimia mwani ikiwemo Kamba na Taitai ili waweze kulima bila ya kikwazo chochote.
Amesema anatambua kuwa Mkoa wa kaskazini Pemba ni maarufu kwa shughuli za uvuvi hivyo, Serikali imejipanga kuwaimarisha kupitia Sekta ya Uchumi wa Buluu kwa kuwapatia Boti za kisasa zenye Mashine na Mitego yenye uwezo mkubwa wa kuvulia Bahari kuu ili kuweza kupata mazao mengi na yenye tija kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.
Amewaahidi kinamama kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya Uongozi wa Rais Dkt. Hussen Ali Mwinyi inatekeleza ahadi zake kwa vitendo kwa kuwasaidia kuwawezesha kupitia vikundi vya ushirika ili kujikwamua kiuchumi hivyo, ni busara wakajiunga katika vikundi vilivyosajiliwa kisheria ili kupata kunifaika na mkpo huo.
Amewatoa hofu juu ya changamoto yao ya hospitali na uchavu wa miundombinu ya barabara kwa kuwaahidi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imedhamiria kuzijenga barabara zote kwa kiwango cha Lami sambamba na huduma muhimu za kijamii ikiwemo Hospitali, Skuli na miundombinu ya maji na umeme.
Akitolea ufafanuzi changamoto ya msitu wa ........ambao wananchi wa kijiji cha Kiungoni wamedai msitu huo kuchukuliwa na wananchi wa Kojani Mhe. Hemed amewanasihi wananchi hao kuacha tofauti zao na waishi kwa umoja na ushirikiano wakati ambao Serikali inatafuta ufumbuzi suala la msitu huo.
Amesema Jimbo la Pandani na Kojani lazima yabaki kwa Chama Cha Mapinduzi katika ngazi zote hivyo umoja na msjikamano kwa wana CCM ndizo nguzo pekee za kuipatia usshindi wa kishindo kwa majimbo yote nchini.
sss
Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Wete Ndg. Hamad Omar Bakari ameeleza kuwa Miundombinu ya Mabomba ya Maji Wilayani humo ni chakavu ambapo Serikali inaandaa mradi wa Maji uitwao Zanzibar Water security Project (ZWSP) ambao upo hatua za awali kuanza kwake ambao utamaliza moja kwa moja tatizo la Maji Pandani na maeneo jirani.
Amesema Wizara ya afya inasimamia ahadi ya Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi kuwajengea Kituo cha Afya kiungoni ambacho tayari mipango ya awali imeshaanza ili kumaliza changamoto inayowakabili wananchi wa eneo hilo kufuata huduma hiyo masafa marefu.
Nae Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kupitia Jumuiya ya Wazazi Bi Habiba Ali Muhamed amewasihi vijana kutumia fursa ya elimu bila ya malipo inayotolewa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili kupata elimu bora yenye manufaa kwao.
Aidha amemshukuru Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwa kuamua kuwafikia wananchi katika ngazi ya majimbo hatua ambayo inaongeza Imani ya wananchi kwa viongozi wao.
Akipokea wanachama wapya Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Ndg. Hemed Suleiman Abdulla amewataka kushikimana na kukiendeleza Chama na kuwaeleza kuwa CCM ni Chama chenye sera zinazotekelezeka kwa maslahi ya wananchi.
No comments:
Post a Comment