Habari za Punde

Vitendo vya Udhalilishaji Vyaongezeka -: Kamishna Hamad

Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Hamad Khamis Hamad akiwa na watoto yatima katika chakula cha pamoja kilichoandaliwa na wadau wa mashairi ikiwa ni shamrashamra kuelekea siku ya tungo njema ambayo hufanyika Kila mwisho wa mwezi wa 9,hafla iliyofanyika Viwanja vya Skuli ya Pongwe Pwani.
Na fauzia Mussa

Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Hamad Khamis Hamad amesema jamii ya wazanzibari ipo pamoja na  watoto mayatima na itaendelea kuwajali   ili na  wao wajisikie kama watoto wengine.

Akizungumza na wadau wa tungo njema  katika hafla ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Redio Al-Nour  kwa watoto hao huko viwanja vya Skuli ya Pongwe Pwani , kamishna Hamadi  alisema mjumuiko huo umeonesha upendo na kuwatia moyo katika safari yao ya maisha.

Amesema watoto  wanakabiliwa na changamoto  nyingi hivyo ipo haja kwa jamii kuwasaidia kutatua changamoto zinazowakabili kwa kuwatia moyo na nguvu ya uthubutu wa kufanya maamuzi sahihi ya kuondokana na vikwazo hivyo.

Akizungumzia vitendo vya udhalilishaji kamishna Hamadi  amesema jamii bado inakabiliwa na changamoto ya ongezeko la vitendo hivyo hususani ubakaji kwa watoto wenye umri kati ya miaka11 hadi 17,hivyo Jeshi la Polisi litaendelea kuwachukulia hatua kali wahusika wa vitendo hivyo.

Alifafanua kuwa kuongezeka kwa vitendo hivyo ni changamoto  kubwa kwa watoto hao inayoleta matokeo mabaya kwa Taifa katika  siku za baadae.

Amesema waathirika zaidi wa vitendo vya udhalilishaji ni watoto ambao wanapitia katika kipindi kigumu cha ukuaji  kutokana na mabadiliko ya maumbile,mabadiliko ya matumizi ya teknolojia,Habari na mawasiliano na Aina mbalimbali za vishawishi wanavyokabiliana navyo.

Alisema takwimu za Jeshi la Polisi Kwa kipindi cha januari hadi Juni 2023 zinaonesha uwepo wa makosa 463 ya ubakaji dhidi ya 212 kwa kipindi kama hicho kwa mwaka  2022 ikionesha ongezeko la makosa 251.

Aidha amewataka wazazi na walezi kuimarisha ulinzi kwa watoto wao ili wapate nafasi ya kuelekea kwenye kutimiza ndoto za maisha yao ya baadae
Sambamba na hayo Alizitaka TAASISI mbalimbali kujitokeza kutoa nyenzo zinazohitajika,fursa na mifumo ya usaidizi ili kuhakikisha watoto hao wanafikia malengo.

Mkurugenzi wa redio Al- Nour Ali Mkubwa Zubeir amesema washairi wa tungo njema  wamekuwa na mchango mkubwa wa kuelimisha jamii  kupitia tungo zao, hivyo kwa kutambua mchango wao  uongozi wa  redio Al- Nour umeweka siku maalum ya washairi hao kuweza kutangaza kazi zao na kujulikana zaidi.

"Sisi redio nuru kwa miaka 13 tumekua tukitumia mashairi yao ,ngonjera na tungo zao katika kuhabarisha,kuelimisha na kuburidisha jamii tukitambua kwamba kazi hio ni ngumu Sana na hatuna cha kuwalipa hivyo umaalum  wa siku hii ni kwa kuthamini kazi zao zinazoakisi na harakati za ujenzi wa Taifa "alifafanua.

Aidha alifahamisha kuwa katika kuwajali mayatima Redio Al-Nour kwa kushirikiana na  wapenzi  pamoja  na wadau wa mashairi wameandaa chakula cha mchana  kwa Lengo la Kuwafariji watoto hao kuelekea siku ya tungo njema.

Akisoma risala ya washairi wa tungo njema Ali Ngome Ali amesema washairi hao wanakabiliwa na uhaba wa nyenzo na kushindwa kumudu gharama za kutolea kazi zao Kwa kiwango kilicho bora na cha kisasa.

Aliongeza kuwa Mbali na changamoto hizo washairi hao wamefanikiwa kupata umaarufu kupitia redio Al-Nour  ambayo inasikika maeneo mbalimbali Bara na Visiwani.

Kwa upande wao  watoto Walioshiriki katika chakula hicho  wamesema wamefarijika kwa  Hafla hiyo na kuwataka wadau na wahisani kujitokeza kuwasaidia zaidi katika Nyanja mbalimbali za kimaenedeleo.

Hafla ya chakula cha mchana kwa watoto mayatima  ni miongoni mwa shamrashamra kuelekea siku ya tungo njema ambayo hufanyika  Kila ifikapo Septemba 30 kwa  Lengo la kutambua na kuthamini juhudi za wasanii wa tenzi na tungo za mashairi kutokana na mchango mkubwa katika  ujenzi wa jamiii iliyobora.
Wanafunzi wa Pongwe Pwani wakisoma utenzi wenye maudhui ya kuwaenzi mayatima katika Hafla ya  chakula kwaajili ya mayatima ikiwa ni shamrashamra kuelekea siku ya tungo njema ambayo hufanyika Kila mwisho wa mwezi wa septemba
Wanafunzi wa Skuli ya Dkt Samia wakisoma utenzi wenye maudhui ya kuwatunza mayatima ikiwa ni shamrashamra kuelekea siku ya tungo njema ambayo hufanyika Kila mwisho wa mwezi wa septemba ,hafla iliyofanyika urowa Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Mtendaji wa Redio Al-Nour Ali Ngome Ali  akisoma risala ya wadau wa tungo njema wakati wa hafla ya chakula cha mayatima iliyofanyika Urowa kuelekea siku ya tungo njema ambayo hufanyika Kila mwisho wa mwezi wa 9
Mkurugenzi wa Redio Al-nuor Ali Mkubwa Zubeir akizungumza na wadau wa tungo njema kabla ya kumkaribisha kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Khamis Hamad Khamis kuzungumza na hao wakati wa Hafla ya chakula kwaajili ya mayatima ikiwa ni shamrashamra kuelekea siku ya tungo njema ambayo hufanyika Kila mwisho wa mwezi wa Septemba hafla iliyofanyika viwanja vya Skuli ya Pongwe Pwani .
Kamishna wa Jeshi la  Polisi Zanzibar Hamad Khamis Hamadi akizungumza na wadau wa  tungo njema wakati wa Hafla ya chakula kwa watoto yatima ikiwa ni shamrashamra kuelekea siku ya tungo njema ambayo hufanyika Kila mwisho wa mwezi wa septemba Urowa
Mkurugenzi wa Redio Al-nuor Ali Mkubwa Zubeir akimkabidhi zawadi maalum kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Hamad Khamis Hamad wakati wa Hafla ya chakula kwaajili ya mayatima iliyofanyika viwanja vya Skuli ya Pongwe Pwani  ikiwa ni shamrashamra kuelekea siku ya tungo njema ambayo hufanyika Kila mwisho wa mwezi wa 9
Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Hamad Khamis Hamad akimkabidhi misahafu  Mkurugenzi wa Redio Al-nuor Ali Mkubwa Zubeir kwa niaba ya  watoto mayatima wakati wa  chakula cha mchana ikiwa ni shamrashamra kuelekea siku ya tungo njema ambayo hufanyika Kila ifikapo mwisho wa mwezi wa 9
Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar  Hamad Khamis Hamadi akimkabidhi albamu ya tungo njema Sheha wa shehia ya Pongwe Pwani Fatma Faki kwaniaba ya mkuu WA wilaya ya Kati Marina Tomas wakati wa Hafla ya chakula kwaajili ya mayatima ikiwa ni shamrashamra kuelekea siku ya tungo njema ambaya hufanyika Kila mwisho WA mwezi wa septemba kwa Kila mwaka
Watoto mayatima wakiwa katika hafla ya chakula iliyoandaliwa na wadau wa mashairi ikiwa ni shamrashamra kuelekea siku ya tungo njema ambayo hufanyika Kila mwisho wa mwezi wa 9,hafla iliyofanyika Viwanja vya Skuli ya Pongwe Pwani.
Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar Khamis Hamad Khamis (alievaa kanzu) akiwa katika PICHA ya pamoja na Kijana Abdillah mwenye ulemavu wa uoni mwenye kipaji cha kusoma nasheed katika hafla ya chakula kwaajili ya watoto mayatima iliyofanyika Uroa Pongwe Pwani.
Wasanii wa mashairi Zero kasorobo na daktari wa mashairi wakitoa burudani ya shairi lenye maudhui ya kuwatunza mayatima katika Hafla ya chakula kwaajili ya mayatima ikiwa ni shamrashamra kuelekea siku ya tungo njema ambayo hufanyika Kila mwisho wa mwezi wa septemba.
Picha na Fauzia Mussa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.