RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, baada ya kumalizika kwa Kisomo na Dua Maalumu ya kumuombea yeye na Viongozi pamoja na Nchi, iliyoandaliwa na Wanazouni na Maimamu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja iliyofanyika katika Msikiti wa Markaz Fisabillilah Tablii Kidoti leo 3-9-2023
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Al hajj Dk. Hussain Ali
Mwinyi amewanasihi waumini wa dini ya kiislamu, wazazi na walezi kwenye jamii
kuhimiza maadili mema kwenye malezi ya vijana wao ili kulinusuru taifa na
athari za mmong’onyoko wa maadili.
Al
hajj Dk. Mwinyi aliyasema hayo Kiodoti Mkoa wa Kaskazini Unguja alikoshirirki
dua ya kuliombea taifa na viongozi wake.
Rais
Dk. Mwinyi alihimiza malezi bora kwa jamii yanayoendana na mila, sila na
tamaduni za asili ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla yanayotokana na misingi ya
dini ili kulinusuru taifa na athari za dawa zakulenya, udhalilishaji, wizi,
uzembe, kubaguana na vijana waliokosa hofu ya kumuogopa Mwenyezi Mungu.
Pia,
Al hajj Dk. Mwinyi alisifu hali ya amani, umoja, mshikamano na maelewano iliopo nchini na kuitaka jamii kuiendelea kuitunza, pia ahimiza udugu na umoja uliopo bila kujali
tofauti zao za kisiasa kwa kutekeleza shughuli za kijamii na kimaendeleo pamoja
na kuwataka waumini wa dini ya Kiislamu kuendeleza utamaduni wa kuliombea dua
taifa na watu wake.
“Ndugu
zangu kila mara nasema na leo napenda nirudie tena katika mambo muhimu katika
nchi yoyote, amani ni jambo la msingi na la kupewa umuhimu wa kipekee, nchi
ikikosa amani hakuna jambo lolote linaweza kufanyika” alilisisitiza Al hajj Dk.
Mwinyi.
Hata
hivyo, Al hajj Dk. Mwinyi aliahidi kutimiza ahadi zote alizoziweka wakati
uchaguzi kuu wa Zanzibar kwa wananchi pamoja na kuyatekeleza mambo muhimu
yaliyokuwa hayako kwenye ahadi zake
nakueleza ni wajibu kwa viongozi kuyatekeleza kwa maslahi ya watu na taifa kwa
ujumla.
Dua
hiyo ya kuliombea taifa ilizishirikisha zaidi ya mardasa 700, viongozi wakuu wa
dini, Serikali pampoja na vyama vya siasa.
IDARA YA MAWASILIANO
IKULU, ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment