Habari za Punde

Haroun afurahishwa na utekelezaji wa Ilani ya CCM katika taasisi zake

Waziri wa Nchi, (OR) ,Katiba,Sheria,Utumisha na Utawala bora  Haroun Ali Suleiman akizungumza na Watendaji wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma wakati wa ziara ya kusikiliza taarifa ya  utekelezaji wa  Ilani ya  Chama Cha Mapinduzi kwa kipindi cha mwaka 2020-2023 ndani ya Taasisi zilizo chini ya Wizara yake.
Katibu wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma  Kubingwa Mashaka Simba akiwasilisha ripoti ya utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa kipindi cha mwaka 2020-2023 ndani ya Ofisi yake wakati wa Ziara ya Waziri wa Nchi, (OR) ,Katiba, Sheria,Utumishi na Utawala bora  Haroun Ali Suleiman  kuangalia utekelezaji huo katika Taasisi zilizo chini ya Wizara yake.

Baadhi ya Watendaji wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma  wakifuatilia uwasilishwaji wa taarifa ya utekelezaji wa  Ilani ya  Chama Cha Mapinduzi kwa kipindi cha mwaka 2020-2023  wakati wa Ziara ya Waziri wa Nchi, (OR),Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala bora  Haroun Ali Suleiman  kuangalia utekelezajio huo katika Taasisi zilizo chini ya Wizara yake.

PICHA NA FAUZIA MUSSA – MAELEZO 

Na Rahma Khamis Maelezo                6/9/2023

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Haroun Ali Suleiman amezitaka taasisi zilizopo chini ya Wizara yake kuwasilisha taarifa za utekelezaji kwa wakati ili ziweze kurahisishwa katika Baraza la Wawakilishi mapema.

 

Ameyasema hayo huko  Ofisi ya Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma katika muendelezo wa  wa ziara katika taasisi zilizo chini  Wizara yake na kuangalia utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi.

 

Amesema wapo taasisi hizo zitatoa taarifa kwa wakati , itasaidia katika utekelezaji wa majukumu yao kwa urahisi na ufanisi hivyo hakuna budi kwa watendaji hao kushirikana ili kufanikisha majukumu hayo.

 

Adha amefahamisha kuwa viongozi wana wajibu wa kufuatilia utendaji  wa kazi katika maeneo husika kwani kufanya hivyo kutapelekea kuepuka malalamiko kwa wananchi na kuyapatia ufumbuzi wa haraka.

 

Hata hivyo wamewataka kuimarisha miondombinu ya kazi ili waeze kufanya kazi wa ufanisi na kuwapongeza  kamisheni ya Utumishi wa umma kwa kutekeleza vizuri majukumu yao.

 

Amesema uwekaji wa kumbukumbu ni kitu muhimu sana kwani kunatoa taaluma ya utunzaji wa kumbukumbu ili kuhifadhi taarifa zisipotee na kusaidia katika utendaji.

 

Aidha amesema ni vyema kwa Viongozi kukutana na wafanyakazi wao mara kwa mara ili kubaini changamoto zinazowakabili na kuzipatia ufumbuzi wa haraka.

 

Mbali na hayo amewataka wafanyakazi kujenga maadili mema katika taasisi taasisi sambamba na kujiendeleza kielimu ili kuongeza ufanisi katika kazi.


Waziri  Haroun ameongeza kuwa tume ya maadili lazima ipange utaratibu maalumu wa kuwafuatilia na kuwasikiliza  wananchi malalamiko yao ili kujenga mustakabali mwema wa taifa.

                

Aidha amewasisitiza wafanya kazi kuendelea kutunza siri za Ofisi kwani utoaji wa siri ni uvunjifu wa maadili katika kazi jambo ambalo linahatarisha maisha ya watu.

 

“Tujitahidini kufuatilia utendaji wetu wa kazi na kutoa taarifa ripoti kwa wakati ili ituondoe malalamiko kwa baadhi ya wananchi kwani tukifanya hivyo tutajenga taifa bora “ ,alisema Waziri.

 

Katika hatua nyengine Waziri aliwapongeza watendaji hao kwa kazi nzuri walioifanya na kuwahimiza  Makamishna kuendelea  kufanya kazi ili kuleta maendeleo katika nchi.

 

Akitoa  taarifa ya utekelezaji ya Ilani ya CCM kwa kipindi cha mwaka 2020_2023 Katibu wa Tume ya maaadili ya Viongozi wa umma Asma Hamid Jidawy amefahamisha kuwa  tume inapokea makamiko ya wananchi na kufanyia uchunguzi na baadae kuyafanyia kazi ili kuondosha usumbufu.

 

Aidha ameeleza kuwa katika kutekeleza ilani ya chama  cha Mapinduzi wameanzisha mfumo maalum ambao unatoa muongozo kuhusu tume ili wanannchi waweze kutuma mashauri yao .

 

Aidha amesema kuwa tume  imefanikiwa kusajili watu 2236 kwa kufanya uhakiki kupitia mfumo huo na kupokea malalamiko 41ikiwemo ya rushwa ,upendeleo katika ajira upungufu wa vifaa vya kufanyia kazina usikilizaji wa mashauri ikiwemo vitisho.

 

Katika ziara hiyo Waziri Haroun ametembelea Ofisi ya Tume ya Maadili ya Viongozi wa  Umma  Vuga na Kamisheni ya Utumishi wa Umma Mwanakwerekwe.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.