Habari za Punde

Jukumu la Usafi wa Jiji ni la wananchi Wote Hivyo Ipo Haja kwa Kila Mmoja Wao Kutimiza Wajibu Wake

Mstahiki Meya wa Jiji la Zanzibar Mahmoud Muhammed Mussa akiongoza zoezi la usafi katika bustani ya Jamhuri, jukumu la usafi wa Jiji ni la wananchi wote hivyo ipo kwa haja kwa kila mmoja wao kutimiza wajibu wake ipasavyo ili jiji liwe safi na haiba  nzuri.

Na.Nafisa Madai.

Mstahiki Meya wa Jiji la Zanzibar Mahmoud Muhammed Mussa amesema jukumu la usafi wa Jiji ni la wananchi wote hivyo ipo haja kwa kila mmoja wao kutimiza wajibu wake ipasavyo ili jiji liwe safi na haiba  nzuri.

Mstahiki Meya Amesema hayo leo alipozungumza na Umoja wa vikundi vya usafi vya Zanzibar mara tu baada ya kumalizika kwa zoezi la usafi katika maeneo ya Jamhuri Gardeni Wellesi na Viwanja vya Maisara ikiwa ni kuelekea katika kilele cha maadhimisho ya siku ya usafi Dunia tarehe 16/9/2023 ambapo kauli mbiu ya Mwaka huu ni “ Usafi shirikishi kwa Utalii endelevu”.

Aidha alisema Baraza la Jiji kupitia Manispaa zake zote wamejipanga kikamilifu katika kuhakikisha Jiji linabaki kuwa safi kwa kuengeza nguvu ikiwemo vitendea kazi na kushirikiana na vikundi vya mazoezi kwa kufanya usafi mara kwa mara katika maeneo mbali mbali ya Jiji la Zanzibar.

Hata hivyo alisema Muelekeo wa Zanzibar hivi sasa ni kuifanya Zanzibar kuwa ni Jiji lenye haiba na mvuto kwa wageni wanaoingia na kutoka na tayari wameanza kufanya kazi na mashirika mbali mbali ambayo wapi tayari kusaidia katika zoezi hilo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Mjini Ndg.Ali Khamis amevishukuru  vikundi hivyo kwa kuandaa zoezi hilo ambapo alivitaka vikundi hivyo kuendeleza utaratibu huo na kuwahikikishia Manispaa Mjini ipo tayar kutoa vifaa vya usafi kila watakapohitaji.

Nae Mwenyekiti wa Huduma Za Jamii wa Manispaa ya Mjini Mhe Muhammed Makame (Laki) amesema kamati yake ipo tayari kuhudumia Vifaa na usafiri kila watakapotaka kufanya zoezi hilo ili kuona Jiji na Manispaa zake zinaenda sambamba katika kutekeleza majumu yao kwa kushirikiana na vikundi hivyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Vikundi vya Usafi Zanzibar Khamis Akhui amesema Cha chao wapo tayari kushirikiana na Manipsaa na Serikali katika kuweka Jiji la Zanzibar safi na wamejipanga kufanya hivyo kila watakapoona kuna uhitaji wa kufanya hivyo.

Imetolea na kitengo cha Habari

BLJ-Zanzibar.

11/09/2023.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.