Habari za Punde

Uvunaji wa matango bahari kisiwani Pemba


Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi, Ofisi ya Pemba, pamoja na wadau wetu wa Shirika la IUCN kwa pamoja tumekuwa tukizidisha juhudi mbali mbali za kuzidisha ubunifu katika ukulima wa mwani na ufugaji wa viumbe maji.

Pichani ni matokeo ya uvunaji wa matango bahari kwa kutumia mtindo wa mashamba jumuishi ya mwani na matango bahari ambayo hivi sasa yamo katika awamu za mbele za majaribio kwa wajasiriamali wetu wa Uchumi wa Buluu.

Ubora wa mavuno haya kisiwani Pemba ni ushahidi wa kutosha wa jinsi gani programu za uwezeshaji za Serikali na wadau wengine wa maendeleo, mbinu bora za ufugaji na ukulima wa mwani, tafiti na vipaumbele vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Sera yake ya Uchumi wa Buluu, vyote hivi vinavyozidi kushamiri

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.