Habari za Punde

Waziri Lela mgeni rasmi katika Mahafali ya 9 ya Chuo cha Mafunzo ya Amali Vitongoji, Chake Chake Pemba

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh. Lela Mohammed Mussa akizungumza machache kabla ya kukabidhi shahada kwa wahitimu wa mafunzo tofauti katika Mahafa;li ya 9 ya chuo cha Mafunzo ya Amali Vitongoji, Chake Chake Pemba
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh. Lela M Chuo cha Mafunzo ya Amali Vitongoji, Chake Chake Pemba ohammed Mussa akimkabishia shahada ya ke ya kuhitimi mmoja wa wahitimu wa


Baadhi ya wahitimu wa Chuo cha Mafunzo ya Amali Vitongoji wakimsikiliza Waziri wa Elimu na mafunzo ya amali alipokuwa akitoa nasaha zake

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh. Lela Mohammed Mussa amesema Wahitimu wa fani mbali mbali kutoka Vyuo vya Amali Nchini ni matunda ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964 ambayoyalipelekea kutangazwa Elimu Bila Malipo ili Wanyonge waweze kunufaika na huduma hiyo.
Mh. Lela ameyasema hayo katika Mahafali ya 9 ya Chuo cha Mafunzo ya Amali Vitongoji Wilaya ya Chake Chake Mkoa wa Kusini Pemba.
Amesema hakuna Nchi yoyote duniani ambayo ilitawaliwa na kutangaza kutoa Elimu bila Malipo kwa Wananchi wake mara tu baada ya kupata uhuru wake kama ilivyofanyika Zanzibar, hivyo kuhitimu kwa Vijana katika fani za kazi za Amali nikuthibitisha jitihada za Serikali za kutoa Elimu Bila ya Malipo.
Mh. Waziri amewataka Whitimu hao kuonesha Uzalendo na kua Mfano bora katika jamii kwa kufanyia kazi fani zao katika kuisaidia jamii.
Akifafanua zaidi Mh. Lela amesema nivyema Wahitimu hao kujitofautisha na Vijana Wengine katika kufanya kazi za taaluma zao ili Waweze kujijengea heshima na Utambulisho (Brand) katika kazi zao.
Nae Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Bi Mwanakhamis Adam Ameir amewataka Wahitimu hao kuwa tayari kuzitumikia taaluma zao kwa Maslahi ya Jamii bila kujali kipato katika hatua za awali.
Amesema kufanya hivyokutawajengea uzoefu na kufanya kazi kwa umahiri jambo ambalo litawafungulia milango ya kupata wateja wengi ambao watapelekea faida kubwa na ya uhakika.
Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Vyuo vya Amali Dkt. Bakari Ali Silima amesema Chuo hicho Kwasasa kinatoa fani sita nakuongeza kwamba Mamlaka inakamilisha taratibu ikiwa nipamoja na Ujenzi wa Miundombinu ili Chuo hicho kiweze kuongeza fani nyengine saba na kufanya jumla ya fani 13.
Aidha Dkt. Bakari amewapongeza Wahitimu hao kwa kubuni Mitindo mbali mbali kupitia fani ya Ushonaji ambapo ameahidi kuwaunga mkono katika kutimiza dhamira yao ya kushona mavazi maalumu ya Wahitimu wa Vyuo.
Awali akisoma risala kwa niaba ya Wahitimu wenzake Mwanafunzi Badria Rashid Khamis ameiomba Wizara ya Elimu kukiangalia kwa karibu Chuo hicho hususan katika eneo la ukarabati wa Miundombinu ili Wanafunzi waweze kujisomea kwa Ufanisi.
Imetolewa na kitengo cha Habari na Mawasiliano(WEMA)

 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.