Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Sultan Ahmed bin Sulayem katika hafla ya Utiaji saini Uwekezaji na Uendeshaji wa Sehemu ya Bandari ya Dar es Salaam iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 22 Oktoba, 2023.
Waziri wa Uchukuzi Mhe. Makame Mbarawa akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Godius Kahyarara wakitia saini Mkataba wa Nchi Mwenyeji baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kampuni ya DP World ya Dubai iliyowakilishwa na Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Sultan Ahmed bin Sulayem kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 22 Oktoba, 2023.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TPA Mhe. Balozi Ernest Mangu akipongezana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya DP World ya Dubai Sultan Ahmed bin Sulayem mara baada ya kusaini Mkataba wa Uendeshaji wa Gati namba 4 mpaka 7 za Bandari ya Dar es Salaam kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 22 Oktoba, 2023.
No comments:
Post a Comment