Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) Mhe. Mama Mariam Mwinyi amewasili leo Bujumbura, Burundi kushiriki katika Jukwaa la Wanawake Viongozi kujadili Mchango wa Uzazi wa Mpango katika kupata Lishe bora na Tija ya Makundi ya watu utakaofanyika kuanzia tarehe 9 hadi 11 Oktoba 2023.
Amepokelewa na Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Burundi Joachim Nyingo na Waziri wa Biashara wa Burundi Mhe.Marie Chantal Nijimbere.
Jukwaa hilo moja ya nyanja za Diplomasia kupitia Wenza wa Wakuu wa Nchi na Serikali kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya nchi zetu mbili.
🗓️07 Oktoba,2023
📍Bujumbura, Burundi.
No comments:
Post a Comment